Bodi
ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii (MAB) yakutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia
Evalist Ndikilo kwa lengo la kutambua mchango wa mkoa na ushirikiano
unaotolewa kwa TFDA katika masuala ya Udhibiti wa Bidhaa za Chakula,
Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa MAB, Balozi Dkt. Ben
Moses, amepongeza ushirikiano uliopo baina ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza na TFDA kanda ya Ziwa na kutoa wito wa kudumisha ushirikiano
uliopo kwa kuwa lengo la udhibiti litafanikiwa ikiwa ushirikiano uliopo
utadumishwa.
'
Naye
Mkuu wa Mkoa amesifu kazi kubwa inayofanywa na TFDA katika kulinda afya
ya wananchi kwani afya za wananchi zikiimarika basi uchumi wa unchi nao
utaimarika. Vilevile, katika kueleza changamoto ambazo mkoa
unakabiliana nazo katika masuala ya udhibiti wa chakula, dawa, vipodozi
na vifaa tiba, Injinia Ndikilo alieleza kuwa usafi katika machinjio ni
changamoto kubwa na kwamba anatarajia kulipatia ufumbuzi hivi karibuni
baada ya kuitisha kikao cha wadau.
Aidha, Injinia Ndikilo ametoa wito kwa TFDA kuona fursa iliyopo ya
kuhamasisha wafanya biashara kujenga kiwanda cha dawa jijini Mwanza
kutokana na idadi kubwa ya wananchi pamoja na kuimarisha udhibiti wa
bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kufuatia kujengwa kwa
kituo cha Biashara cha Jiji la mwanza ambapo milango ya biashara nyingi
itakuwa wazi hususan bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA.
Wajumbe wakiendele a na mazungumzo Yao na Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Injinia Ndikilo, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya TFDA ofisini kwake.
0 comments:
Post a Comment