Na John Maduhu, Mwanza
MTANDAO wa Uendelezaji na Ukuzaji wa Biashara na Bidhaa zinazozalishwa Tanzania (TAN TZ) umeiomba Serikali kuliandaa Jiji la Mwanza liweze kuwa soko la bidhaa kwa ajili ya nchi za maziwa makuu.
Akizungumza mjini hapa jana katika Maonyesho ya Bidhaa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mkurugenzi Mkazi wa TAN TZ, Deusdedit Kizito, alisema Mwanza inafaa kwa ajili ya kutumika kama soko muhimu kutokana na kuwa katikati ya nchi za maziwa makuu.
Alisema endapo Mwanza itakuwa soko muhimu kwa nchi za maziwa makuu, bidhaa zinazozalishwa nchini zitaweza kutawala katika masoko ya nchi za EAC na kuinua uchumi wa Tanzania.
“Katika maonyesho haya ya TAN TZ tumeweza kusaidia vikundi 30 toka katika mikoa 10 hapa nchini, endapo maonyesho haya yakiboreshwa zaidi na kupatikana bidhaa bora Tanzania itaweza kuteka soko la maziwa makuu kwa kuwa katika nchi zilizoshiriki katika maonyesho haya bidhaa za Tanzania zimekuwa zikipata soko zaidi ya bidhaa toka kwa nchi jirani,” alisema Kizito.
Aliwataka wazalishaji wa Tanzania kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kulitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha linadhibiti bidhaa ambazo ziko chini ya kiwango.
Naye, Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani, Baltazar Kitundu, alisema wataendelea kuwajengea uwezo wazalishaji wadogo wa Tanzania kwa kushirikiana na TAN TZ.
Alisema wamekuwa wakitoa msaada wa fedha na mafunzo kwa wajasiriamali wa Tanzania, waweze kuboresha bidhaa zao na kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya kimataifa ya biashara yanayofanyika ndani na nje ya Tanzania.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment