Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgeni
rasmi, Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi.
Esperance Makuza,aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza
akifungua warsha ya siku tatu ya watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini
Mwanza Jumanne Novemba 28,2017.
Afisa
Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona
akielezea historia ya shirika la AGPAHI na shughuli zinazofanywa na
shirika hilo nchini Tanzania.
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa.
Mwezeshaji Gladness Olotu akiendelea kutoa mada ukumbini.
Shirika
la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI)
linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI
limetoa warsha kwa Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza ili kuwajengea
uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo
(CTC).
Warsha
hiyo ya siku tatu iliyoanza siku ya Jumanne Novemba 28,2017 katika
ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza imekutanisha WAVIU washauri
kutoka halmashauri za wilaya za
Ilemela,Kwimba,Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana.
Waviu
washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na
wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa
wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha
sambamba na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na
kupunguza unyanyapaa.
0 comments:
Post a Comment