Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Lazaro Twange (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitanda vya kujifungulia akina mama kwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vincent Naano (kulia).
TPA
imekabidhi jumla ya vitanda saba (7) vya kujifungulia akina mama pamoja
na vyandarua mia tatu (300) kwa hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Musoma
iliyopo Mkoa wa Mara.
Hafla
fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba hivyo vyenye thamani ya Sh. Milioni
15 imefanyika Jumatatu Oktoba 02, 2017 hospitalini hapo ambapo
mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA alivikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya
Musoma.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo Naibu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA,
Bw. Lazaro Twange amesema msaada huo ambao umetolewa na TPA ni sehemu ya
jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za
kuboresha sekta ya huduma za afya.
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vincent
Naano ameishukuru TPA kwa kuacha shughuli zake nyingine muhimu na kuamua
kutoa msaada huo mkubwa kwa Mkoa wa Mara.
“Msaada
huu hautatumika kwa hospitali kuu tu bali utasambazwa kwa vituo vingine
vya afya vya bweri, nyasho, mwangi na nyamatare ambako utasaidia
kupunguza idadi ya wagonjwa wanaofika hospitali kuu kwa kukosa huduma
vituoni” amesema Dk. Naano.
Ameongeza
kwamba Wilaya ya Musoma inashirikiana kwa karibu na Mamlaka mbalimbali
katika kuwaletea Wananchi wake maendeleo na kukumbusha kwamba mwaka juzi
(2015) TPA iliisaidia Wilaya yake kwenye ununuzi wa madawati na sasa
imesaidia sekta ya afya na kuwaasa wadau wengine kujitokeza kusaidia
hasa katika ujenzi wa madarasa ambao kuna upungufu mkubwa.
Sera
ya TPA ya misaada kwa jamii inalenga katika kuchangia huduma za Afya,
Elimu na Maendeleo ya Jamii ambapo katika kipindi cha mwaka 2016/2017,
yatari Mamlaka imetoa msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 75 kwa
bandari zilizopo kwenye Ziwa Victoria pekee.
0 comments:
Post a Comment