Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Naibu Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika kikao na ujumbe wa wataalamu wa Sekta ya Nishati toka nchini Uganda na Tanzania waliompatia taarifa ya maendeleo ya utafiti wa mafuta katika bonde la bonde la ufa ya Eyasi Wembere la Ziwa Tanganyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017. Picha na IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kufanikisha utafutaji na
upatikanaji wa mafuta yaliyopo katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa
Tanganyika hapa nchini ili Tanzania ianze kunufaika na rasilimali hiyo.
Mhe.
Rais Magufuli amesema hayo leo muda mfupi baada kupokea taarifa ya
maendeleo ya utafiti wa mafuta katika maeneo ya bonde la ufa ya Eyasi
Wembere na ziwa Tanganyika, iliyowasilishwa na timu ya wataalamu wa
Tanzania na Uganda.
Timu
hiyo imeelezea uwepo wa viashiria vya uhakika vya kijiolojia
vinavyothibitisha kuwepo kwa mafuta katika maeneo ya Senkenke, Mwanzugi
na Kining’inila katika bonde la Manonga, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani na Balozi wa
Uganda hapa nchini Mhe. Richard Kabonero, timu ya wataalamu hao imesema
miamba, uoto na uwepo wa bonde Eyasi Wembere katika mfumo mmoja wa bonde
la Afrika Mashariki unaofanana na maeneo mengine yaliyothibitika kuwa
na mafuta ni kiashiria muhimu cha kuwepo mafuta.
Kufuatia
taarifa hiyo Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo
tayari kutekeleza shughuli zote zitakazowezesha kupatikana kwa mafuta
katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika na amewaagiza wataalamu
wa Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wataalamu wa Uganda
ambao wana uzoefu wa kupata mafuta katika ziwa Albert nchini humo.
Mhe.
Rais Magufuli amewashukuru wataalamu wa Uganda wanaoshirikiana na
wataalamu wa Tanzania katika kazi hii na amemuomba Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini wa Uganda Bw. Robert Kasande kumfikishia
shukrani zake kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa
ushirikiano anautoa kwa Tanzania katika kufanikisha upatikanaji wa
mafuta ya nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment