Tone

Tone
Home » » KIJANA RUYENDELA KUTOKA JIJINI MWANZA ANAOMBA MSAADA

KIJANA RUYENDELA KUTOKA JIJINI MWANZA ANAOMBA MSAADA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kushoto ni Naibu katibu mkuu wa taasisi ya kutetea Haki Za Binadamu Tanzania (TAHURA) akifanya Mahojiano na kijana Ruyendela Barugali.( Kulia),Kijana ambaye anahitaji msaada wa rais Dkt.John Magufuli picha David John

Na David John Mwanza

KIJANA Ruyendela Barugali mkazi wa Nyamagana mkoani Mwanza anamuomba rais Dkt. John Magufuli kumsaidia kwani anaishi katika mazingira magumu na amepotezana na mama yake mzazi tangu akiwa mdogo.

Pia baba yake mzazi alishafariki miaka mingi hivyo anamkumbuka rais Magufuli kwani kuna wakati aliwahi kuzamia na Treni hadi Dar es Salaam ambapo aliwahi kupewa sh 20000 katika eneo la Magomeni wilaya ya kinondoni wakati huo akiwa waziri wa Ujenzi.

Ruyendera Ameyasema haya leo jijini Mwanza katika eneo la Makoroboi ambapo maisha yake yote yanapatikana hapo ambapo anamiaka kumi analala nje huku akisema hapendezwi na hali hiyo .Amesema kuwa kimsingj hapendi maisha anayoishi na anatamani kuona rais wake John Magufuli anamsoma ili aweze kumsaidia huku akidai kutokana na ngumu aliyonayo anatamani kusoma lakini hayupo mtu wa kumshika mkono.

"Simjuwi mama yangu niliwahi tu kuwaambiwa kwamba mama yangu anaitwa Zawadi na nasikia anaishi Nyarugusu.na baba yangu mkubwa anaitwa Kanyikalila Mtalemwa anaishi Mganza wilayani chato. "amesema Ruyendela .Pia anasema baba yake alishafariki siku nyingi tangu yeye akiwa mdogo na kudai bahati mbaya aliyonayo hana ndugu wa jamaa hali inayomfanya kuonekana kama mtoto wa mtaani.

Anasema msaada pekee anaouna ni rais Dtk John Magufuli kwani anasema kwakuwa alishawahi Kumsaidia na akamtaka arudi chato mkoani Geita na akafanya hivyo lakini bahati mbaya mazingira aliyokutana nayo kwa baba yake mkubwa Mzee Kanyikali yalikuwa sio rafiki.

Pia ameomba viongozi na wadau wengine kujitokeza kumsaidia kwani hata maeneo anayolala anasumbuliwa na polisi kila wakati hali ambayo inamhuzunisha nakusababisha amkumbuke mama yake.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa