Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rutala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza juu ya utunzaji wa miradi ya maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akipata taarifa kuhusu miradi ya maji wilayani Ukerewe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa tenki la maji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa mashine za kusukumia maji.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewataka wananchi
wa wilaya ya Ukerewe kutunza miradi ya Maji kwa kuwa serikali
inaigharamia kwa fedha nyingi.
Jafo aliyasema hayo alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa Kazilamkanda ambao utahudumia vijiji vipatavyo 13 wilayani humo.
Amesema
serikali inafanya jitihada za kuwatatulia wananchi wake kero mbalimbali
ikiwemo ya upatikanaji wa huduma ya maji, hivyo ni vyema wakatunza
miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Akikagua
mradi huo, Jafo alimpongeza Mkandarasi aliye jenga chanzo na tanki la
kuhifadhia maji la lita 680,000 ambaye ni Lutare Make Enginnering Ltd
kwa kazi nzuri.
Amesisitiza kukamilishwa kwa usambazaji wa Maji katika vijiji vyote 13 kabla ya Disemba 30 mwaka huu.
Naibu
Waziri huyo amesisitiza kulazwa mabomba yaliyo na ubora ili kuepusha
kupasuka kwa mabomba endapo mabomba hayo yatakuwa hayana viwango na
kusababisha hasara kubwa kwa wananchi na halmashauri baada ya
kukabidhiwa mradi husika.
0 comments:
Post a Comment