Tone

Tone
Home » » MWEKEZAJI ASUBIRI ENEO AFUGE SAMAKI

MWEKEZAJI ASUBIRI ENEO AFUGE SAMAKI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SERIKALI ya Kijiji cha Kasenyi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza inasuburi kuridhia kutoa eneo kwa mwekezaji ili kuanzisha mradi wa kufuga samaki ndani ya ziwa Victoria.
Mradi huo mpya wa kufuga samaki utakaogharimu Sh milioni 150 ulibuniwa na Sebastian Slivel baada ya kutembelea na kujifunza katika miradi hiyo Jinja, Uganda.
Silvel ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, alisema tayari amenunua vifaa vya kutosha zikiwamo nyavu na mapipa vitakavyotumika kujenga mradi katika eneo lenye ukubwa wa kilometa moja ndani ya maji ya ziwa Victoria.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kasenyi, Ibrahimu Kabonde alisema wiki ijayo kitaitishwa kikao cha mkutano mkuu wa kijiji ili kupata maoni ya wananchi kabla ya kuingia mkataba wa mradi huo.
Mkuu wa Idara ya Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Abubakar Rutta alisema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa tofauti na miradi ya kufuga samaki kwenye mabwawa ya nchi kavu yenye gharama kubwa za uendeshaji.
Akifafanua alisema kati ya mwaka 2012 hadi sasa yamejengwa mabwawa 64 na kati ya mabwawa hayo, 34 yamejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Kuhifadhi Mazingira ya ziwa Victoria (LVEMP).
Mwenyekiti wa kikundi cha kufuga samaki cha kijiji cha Bugula, Juma Mfaume alisema mradi wao wa mabwawa 12 ulianzishwa mwaka 2013 kwa ufadhi wa LVEMP haujawa na tija kwa sababu ya kukosa maji.
Mratibu wa mradi huo, Justin Nazi alisema jamii imehamasika na shughuli ya kuchimba mabwawa mapya 10 inaendelea katika vijiji vya Hamkoko, Nakatungulu, Msozi na kisiwani Ukara.
CHANZO :HABARI LEO  

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa