Na
Godfriend Mbuya
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Lameck Nchemba amelitaka jeshi la polisi
kanda ya ziwa kuendelea kupambana na matukio ya kihalifu ambayo yameshamiri
katika maeneo yao.
Waziri
Nchemba ameyasema hayo Jijini Mwanza baada ya kupokea taarifa na kusikiliza
kero mbalimbali za wafanyakazi walio katika wizara yake pamoja na kupokea
taarifa juu ya ulinzi na usalama kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mwanza Ahmed
Msangi.
“Endeleeni
kupambana na matukio yote ya uhalifu, matukio ya uvuvi haramu, mauaji ya albino
na vikongwe pamoja na matukio ya ujambazi ili kuhakikisha maeneo yenu yanakuwa
salama katika kazi mbalimbali halali za watu” Amesema Waziri Nchemba.
Aidha
Waziri Nchemba ametembelea makazi ya askari polisi katika eneo la Mabatini
pamoja na Igogo na kuona hali halisi ya uchakavu na ubovu wa makazi hayo na
kulitaka jeshi la polisi kwa kazi ambazo zipo chini ya uwezo wao kutumia nguvu
kazi iliyochini yao.
Pamoja
na hayo Waziri Nchemba amelitaka Shirika la Umeme nchini TANESCO kutowakatia
umeme taasisi zilizochini yake badala yake madeni yote yapelekwe makao makuu ya
TANESCO na baada ya hapo yawasilishwe Wizara ya Fedha ili malipo yaweze
kufanyika kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment