MADIWANI wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela wamepitisha Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza.
Mpango huo utahakikisha jiji na manispaa, zimepangwa kisasa kuondoa migogoro na kuongeza kasi ya ukuaji wa kiuchumi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa wadau wa mpango huo hivi
karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema kuwa rasimu ya
mpango huo, inahusisha mikakati na mapendekezo kutoka sekta tatu za
maendeleo ya mji ambazo ni matumizi ya ardhi, usafirishaji na
miundombinu.
“Huu ni mkutano wa sita wa mapendekezo ya rasimu ya mpango kabambe wa
jiji la Mwanza na wa mwisho ili kuwa mpango kamili utakaotumika katika
jiji la Mwanza kama sheria,” alisema Mongela.
Mongela alisema mpango huo wa kina wa matumizi ya ardhi, utatumiwa
kama kichocheo cha kujumuisha ardhi inayohitajika kwa mapendekezo ya
maendeleo mbalimbali katika sekta za usafirishaji na miundombinu.
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment