Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, akizungumza katika
uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.
Wananchi wa Kata ya
Mabatini Jijini Mwanza, wametakiwa kuunda na kusajili vikundi vya Kijamii kwa
ajili ya kupata fursa ya kusaidiana katika shughuli mbalimbali ikiwemo maafa.
Diwani wa kata hiyo, Deus Lucas Mbehe (Chadema), alitoa rai hiyo
juzi katika uzinduzi wa Kikundi cha kusaidiana cha Ushirikiano Peoples,
kinachoundwa na wanachama wa Chadema kata ya Mabatini.
"Kupitia
vikundi hivyo, wanajamii wataweza kusaidiana
katika matatizo yanayojitokeza katika jamii ikiwemo misiba pamoja na
kusaidiana
kiuchumi kwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali katika vikundi vya
kijamii ambapo nawasihi msiingize ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo udini
na itikadi za
kisiasa katika vikundi hivyo". Alisema Mbehe.
Abdallah Mkama ambae ni Katibu wa Kikundi cha Ushirikiano Peoples,
aliwahimiza wananchi wa Kata ya Mabatini kujiunga na kikundi hicho ili kwa
pamoja kuendeleza ushirikiano uliopo katika masuala mbalimbali ikiwemo starehe
na maafa.
Kwa upande wake Salma Ibrahim ambae ni Mwenyekiti wa Kikundi
hicho, alitanabaisha kwamba matarajio ya
kikundi hicho ni kufanikiwa zaidi hususani katika kuinuana kiuchumi mbali na
kusaidiana katika maafa na starehe.
Uzinduzi wa kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 100
uliambatana na harambee ya kukiimarisha kikundi ambapo zaidi ya shilingi
milioni moja zilipatikana kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa mapungufu yaliyopo
ambayo ni ununuzi wa viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200.
0 comments:
Post a Comment