Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (kulia) akijadili jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) na Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Dkt. Dalaly Peter Kafumu nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuwasilishwa kwa makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji 2016/2017 leo.
Na.Aron
Msigwa- MAELEZO.
Serikali
imesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itatekeleza mradi wa maji katika
vijiji 100 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu la maji linalotoka ziwa Victoria
hadi Kahama na Shinyanga ili kuwawezesha wanachi wanaoishi katika vijiji hivyo
kupata huduma ya maji safi na salama.
Akizungumza
Bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
amesema kuwa mradi wa kuvipatia maji vijiji hivyo utakwenda sambamba na
uboreshaji wa huduma ya maji kwenye vijiji 40 vilivyotambulika katika
Halmashauri za Misungwi, Kwimba, Shinyanga na Msalala.
Amesema kazi
ya kupima na kufanya usanifu wa miradi katika katika vijiji hivyo vya
Halmashauri ya Msalala na Shinyanga imeanza na gharama yake imekadiriwa kufikia
shilingi bilioni 2.59 huku akiongeza kuwa hadi machi, 2016 ujenzi wa miradi ya
maji umekamilika katika vijiji 11 vya Halmashauri hiyo.
Mhe.Lwenge
amesema katika mwaka wa bajeti 2016/2017 Wizara yake itakamilisha ujenzi a
miradi ya maji katika Halmashauri za wilaya za msalala na Shinyanga na kuanza
Usanifu wa miradi hiyo kwenye Halmashauri za Kwimba na Misungwi ambapo kiasi cha shilingi milioni 760.67
kimetengwa kwa kazi hiyo.
Amevitaja
baadhi ya vijiji ambavyo sasa wananchi wake wanapata maji safi na salama
kufuatia kukamilika kwa miradi hiyo kuwa ni Nyashimbi, Magobeko, Kakulu,
Butegwa, Ngihomango, Jimodoli, Kadoto,Lyabusalu ,Mwajiji Ichongo na Bukamna.
Katika hatua
nyingine Mhe.Lwenge amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa
kushirikiana na Serikali ya Ubelgiji itatekeleza mradi mkubwa wa maji
utakakaowawezesha wananchi Laki mbili (200,000) wa Halmashauri zote za mkoa wa
Kigoma kupata maji safi na salama.
Amesema mradi
huo unatarajia kugharamia kiasi cha Euro milioni 8.8 ambapo kati ya fedha hizo
Euro milioni 8 zitatolewa na Serikali ya Ubelgiji na fedha iliyobaki itatolewa
na Serikali ya Tanzania.
Ameongeza kuwa
vijiji 26 vya kipaumbele vya mkoa wa Kigoma vimeainishwa kwa ajili ya kuanza
utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa
wizara yake tayari imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni 5.28 zote zikiwa ni
fedha za nje kwa ajili ya utekelezaji wa
mradi huo.
Pia amesema
Serikali katika mwaka wa 2016/2017 wa fedha imetenga kiasi cha shilingi bilioni
1 kufanyia ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya maji ili kuzipatia maji kata
saba za wilaya ya Masasi zenye idadi ya watu
84,082.
Aidha, amesema
katika mwaka huo wa fedha serikali itatekeleza mradi wa kutoa maji mto Ruvuma
kuyapeleka Mtwara –Mikindani pamoja na vijiji 26 vitakavyopatikana kilometa 12
kutoka eneo la bomba kuu.
Mradi huo
utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya China
kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 189.9 ambapo kazi ya ujenzi wa chanzo
kutoka mto Ruvuma , Chujio la kutibu maji , nyumba ya kusukuma maji , matanki
26, tanki kuu la ujazo wa lita milioni 30 litakalojengwa eneo la maghamba.
Aidha, vituo
vya kuchotea maji 234 na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali kilometa
63 yatajengwa ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 9 hadi lita
milioni 120 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya watu na viwanda mbalimbali
vinavyojengwa vikiwemo vya Saruji na Gesi.
0 comments:
Post a Comment