Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imesema hali ya ubora wa maji si nzuri kwa sababu sio sehemu zote zina miundombinu ya kutibu maji.
Kauli hiyo ilitolewa juzi Mjini hapa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mbogo Futakamba wakati wa kukabidhiwa cheti cha Ubora maabara ya Mwanza.
“Kuna maeneo mengine utakuta kuna madini kwenye maji lakini tunashirikiana na watu wa nje ya nchi kubaini maeneo hayo, na kwenye maeneo ambayo hatujaweka mashine za kutibu maji watu wachemshe,” alisema.
Alisema kwenye maeneo ambayo Wizara ya Maji imehusika katika kujenga miundombinu ya maji hali ya kutibu maji ni nzuri. Futakamba alisema Mwanza imepata cheti cha kuonesha kiwango cha kimataifa cha huduma ya maji.
Maabara hiyo imeweza kufikia vigezo 15 vya kimataifa na itasaidia kupima ubora wa maji.
Alisema mpaka sasa nchini kuna maabara 16 za maji na wataendelea kuboresha maabara nyingine ili ziweze kupata ubora kwa matumizi ya maji na kuongeza “Sasa kupitia maabara ya Mwanza tunaweza kuhudumia watu wa ndani na nje ya nchi na tutatathimini vigezo mbalimbali na hata wataalam wa utafiti wanaweza kuja”.
Alisema maabara ya Mwanza imeweza kufikia vigezo vya ubora kimataifa kutokana na kupata msaada kutoka Mradi wa uhifadhi wa mazingira ambavyo vifaa vya kupitia hatua zote zilipatikana.
Kwa upande wake mtaalam kutoka Shirika la Viwango Nchini (TBS), Stella Mroso alisema maabara ya Mwanza imepata umahiri kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa.
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment