Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo ametaka Mamlaka ya
Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA) kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya
wafanyakazi hasa utoaji wa mafao kwa wastaafu.
Pia, Ndikilo alisema SSRA inapaswa kuchukua
changamoto zote zilizotolewa na wafanyakazi kwenye sherehe za Mei Mosi
ambazo kimkoa zilifanyika viwanja vya CCM Kirumba, kwani wengi walidai
baadhi ya mifuko kutoa mafao kidogo.
Akifungua mafunzo ya utoaji elimu kwa wafanyakazi
wa halmshauri za Mkoa wa Mwanza jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhandisi
Evarist Ndikilo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Warioba Sanya alisema
changamoto za mifuko ya jamii zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi kuondoa
malalamiko ya wafanyakazi.
“Kumekuwa na malalamiko mengi ya wafanyakazi hasa
kwa mifuko ya hifadhi ya jamii, naomba SSRA mfanye jitihada kuhakikisha
malalamiko hayo yanakwisha ili watumishi wanapostaafu wapate mafao bila
matatizo,” alisema Ndikilo na kuongeza:
“Mifano hai tuliiona kwenye sherehe za wafanyakazi
CCM Kirumba, kulikuwa na malalamiko mengi yanayohusu mifuko ya jamii
ikiwamo kutoa mafao kidogo kwa wastaafu, hivyo naomba suala hilo
litafutiwe ufumbuzi mapema.”
Ndikilo alisema kumekuwa na malalamiko ya utoaji
mafao yanayotofautiana, jambo hilo linaibua kero kwa wafanyakazi hivyo
ni vyema likatazamwa kwa undani.
“Kama mtafanya jambo hilo mtakuwa mmewasaidia, watumishi wote wa umma watanufaika na mifuko hiyo,” alisema Ndikilo.
Mwelimishaji kutoka SSRA, Sarah Kibonde alisema
kumekuwa na tatizo la watu kutokujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,
jambo ambalo ni changamoto kwani idadi ya wanachama ni ndogo.
“Mpaka sasa takriban watu milioni 1.8 ndiyo
wamejiunga na mifuko ya jamii, nia yetu ni kuhakikisha tunatoa huduma
bora kwa Watanzania, hivyo sote tujiunge na mifuko hiyo kwa faida yetu,”
alisema Kibonde.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment