Tone

Tone
Home » » DAKTARI BINGWA WA UGONJWA WA SARATANI YA MATITI KUTOKA BANGAROLE INDIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA MISHENI YA WILAYA YA SENGEREMA NA BUGANDO JIJINI MWANZA‏

DAKTARI BINGWA WA UGONJWA WA SARATANI YA MATITI KUTOKA BANGAROLE INDIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA MISHENI YA WILAYA YA SENGEREMA NA BUGANDO JIJINI MWANZA‏



 DAKTARI bingwa wa ugonjwa ya saratani ya matiti kutoka Bangarole India, Profesa Anthony Pais, amewataka madaktari nchini kuunganisha nguvu kukabiliana na ugonjwa huo ambao umekuwa tishio na unaogharimu maisha ya watu kwa kiasi kikubwa.

“Ugonjwa huu kwa sasa unatishia maisha ya binadamu kwa kasi kubwa kuliko ilivyokuwa zamani. Hivyo juhudi zinahitajika sasa kuukabili bila kuchelewa,”

 Pais alisema hayo jana alipokuwa akiongea na madaktari na viongozi wengine wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando Jijini Mwanza. Amesema kuwa yeye yuko tayari kuanzisha mchakato wa ushirikiano huo ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu kuona kuwa wagonjwa wa saratani wanatibiwa hapa nchini badala ya kusafirishwa kwenda India kufuata matibabu hayo kwa gharama kubwa.

Daktari huyo bingwa yupo nchini kutembelea hospitali kadhaa kujionea ukubwa wa tatizo linalosababishwa na ugonjwa huo wa saratani hapa nchini na kuona uwezekano wa kujenga kituo cha uchunguzi wa ugonjwa huo. Ziara hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Limited, yenye haki pekee ya kusambaza vinywaji cha Windhoek Larger , Windhoek Draught na kinywaji kisicho na kilevi cha Climax hapa nchini.

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa kampuni hiyo James Rugemalira alieleza kuwa kampuni yake ilishitushwa na kuenea kwa ugonjwa huo kwa kasi hapa nchini ambapo kila siku watu wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

 Hivyo alisema kuwa kampuni yake iliona umuhimu wa kufanya kila linalowezekana kutafuta njia za kukabiliana na ugonjwa huo bila kuchelewa.

 Profesa Pais tayari ametembea Dar es Salaam, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean Road, Dodoma, Singida, Kahama, Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo, Hospitali ya Misheni ya Kagondo, Bukoba ambapo alizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya afya, wakiwemo wanachama wa klabu ya Rotary ya mkoa wa Bukoba, kuhusu mchakato huo wa ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa saratani ya matiti hapa nchini.

Naye Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya saratani katika hospitali hiyo, Dk. Nestory Masalu, alimshukuru daktari huyo kutoka India kwa kubuni wazo hilo kwa madaktari kuunganisha nguvu, kwani ndiyo itakayo kuwa njia pekee ya kupambana na ugonjwa huo unaogharibu maisha ya watu kila kukicha.
Profesa Pais (kulia), akizungumza na madaktari viongozi na madaktari wa Hospitali ya Bugando. Kutoka kushoto ni Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Saratani wa hospitali hiyo Dk.Beda Likonda na Respicius Didace aliyeongoza na msafara wa Profesa Pais. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Profesa Pais (wa pili kulia), akizungumza na madaktari ha wa Hospitali ya Misheni ya Sengeremao. Kutoka kushoto ni Ofisa Msaidizi wa Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo Daniel Mihayo, Mganga wa hospitali hiyo, Chacha Ernest, Dk.Fred Limbanga ambaye yupo katika msafara wa Profesa Pais na 
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira na Respicius Didace. Profesa Pais yupo nchini kwa ziara maalumu ya kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya afya kuona uwezekano wa kujenga kituo cha uchunguzi wa ugonjwa wa saratani ya matiti kwa mualiko wa James Rugemalira.
Ofisa Mawasiliano wa Kimataifa na Maendeleo wa Hospitali ya Bugando, Josephine Mkono (kulia), akizungumza na Profesa Pais na ujumbe wake na madaktari wa hospitali hiyo.
Profesa Pais (wa tatu kushoto), ujumbe aliongoza nao na madaktari wa kitengo cha ugonjwa wa saratani wa hospitali ya Bugando wakiwa mbele ya jengo jipya la saratani linaloendelewa kujengwa hospitalini hapo.
Muuguzi wa Hospitali ya Misheni ya Wilaya ya Sebgerema, Oliver Mathias, akimuhudumia mtoto aliyelazwa kwa matibabu katika hospitali hiyo wakati Profesa Pais alipotembea hospitalini hapo. Kulia ni mama wa mtoto huyo.
Moja ya Jengo la Hospitali ya Misheni ya Wilaya ya Sengerema linavyoonekana.
Jengo jipya la saratani linalojengwa katika Hospitali ya Bugando linavyooneka.
Jengo la Hospitali ya Bugando linavyoonekana kwa mbele.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa