Tone

Tone
Home » » PINDA AUNGWA MKONO UGOMBEA URAIS

PINDA AUNGWA MKONO UGOMBEA URAIS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza nia yake ya kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2015, baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wameunda mtandao maalum wa kumfanyia kampeni.
Taarifa za uhakika ambazo NIPASHE Jumapili imezipata, zinasema hatua hiyo imefikiwa kutokana na kumuunga mkoni imani waliyo nayo, wakisema anakidhi haja na vigezo.

Harakati hizo zimeanzia ndani ya Bunge hilo na zinafanyika kwa siri kubwa wakati Pinda mwenyewe ikidaiwa kutokuwa na habari za kuwapo kwa kampeni hizo.

Hivi karibuni akiwa jijini Mwanza, Pinda, alitangaza nia yake hiyo akisema alifikia uamuzi huo kufuatia maombi ya viongozi mbalimbali, wa kidini na kijamii wakimtaka kufanya hivyo.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao, baadhi ya wabunge hao walilieleza NIPASHE Jumapili kuwa wamefurahishwa na hatua hiyo ya Pinda na kuahidi kumfanyia kampeni wakati utakapowadia.

WABUNGE KANDA YA ZIWA NA KUSINI
Mmoja wa Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga alisema kutokana na kutokuwa na kashfa ya aina yoyote ambayo inaweza kutolewa kuwa kikwazo kwake kugombea nafasi hiyo, haitawawia vigumu  kumnadi Pinda mbele ya wapiga kura.

“Sisi wabunge kutoka kanda ya ziwa tumeungana kuhakikisha dhamira ya Pinda inatimia,” alisema mbunge huyo machachari kutoka mkoani Shinyanga.

Naye mbunge kutoka mkoani Rukwa, alisema uamuzi wao wa kumuunga mkono Pinda siyo tu unakusudia kubakiza CCM madaraka bali wanataka Tanzania ipate Rais asiyekuwa na makundi.

“Huyu mzee akitimiza dhamira yake kutakuwa hakuna makundi, kila mtu atabaki salama, kuliko tukifanya maamuzi mengine,” alisema.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mbunge kutoka Kanda ya Kusini, ambapo alisema mtindo wa uongozi usiojali urafiki, kurudisha fadhila na kuangalia taifa kwanza, ndicho kitu pekee kilichomvuta kujiunga na kundi hilo.

Alisema kwenye chombo hicho, idadi kubwa ya wabunge imeegemea kwa Waziri Mkuu huyo tangu atangaze nia yake.

“Ukweli ulio wazi ni kwamba katika majina yote, la Pinda ndio limekuwa midomoni mwa wajumbe, lakini tumekuwa na uoga kuzungumza kutokana na chama kutuzuia,” alisisitiza.

Alisema wengi wao wanaamini katika nafasi aliyonayo kama waziri mkuu, amefanya kazi kwa asilimia 60 ya uwezo wake, hivyo wanahitaji utendaji wake wa jumla.
Aliongeza kuwa katika nafasi yake ameonyesha jinsi msaidizi wa Rais anatakiwa kuwa, ambapo amekuwa mtiifu na hata kama kuna kosa anajaribu kulichukua yeye.

Pinda anaongeza idadi ya watu wanaotajwa kutaka kuwania nafasi hiyo wakiwamo Mawaziri Wakuuwastaafu, Edward Lowassa na Federick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernad Membe.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa