Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI
wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Mkoa
wa Mwanza, Pendo Ojijo, amewataka wanawake nchini kuachana na dhana ya
kukikumbatia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika masuala mbalimbali kwani
kipo mstari wa mbele katika kuliteketeza Taifa la Tanzania.
Alisema wanawake ni jeshi kubwa lisilojitambua na kwamba, wakiamua
kutumia nguvu walizonazo wanaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi
na kisiasa ndani ya nchi.
Ojijo, alitoa kauli hiyo juzi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika
kata ya Nyambiti Wilaya ya Kwimba na Magu Mjini mkoani Mwanza.
Alisema licha ya wanawake kuwa waathirika wakubwa wa kushindwa
kuwahjibika kwa serikali iliyopo madarakani, pia ndiyo wamekuwa
wakikiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kwa matumaini ya kupewa kanga na
fulana siku ya uchaguzi.
“Wanawake tumekuwa wahanga wakubwa kutokana na serikali ya CCM
kushindwa kutekeleza wajibu wake, tunafurahia kanga na kofia
tunazoletewa siku ya uchaguzi na kukubali kuteseka kwa muda wa miaka
minne baada ya kuwaweka madarakani watu wasiojali matumizi bora ya
rasilimali za nchi,” alisema Ojijo.
Alisema viongozi waliyopo madarakani kwa sasa, wamekosa utu, uzalendo
na hata moyo wa kuijali Tanzania, hali inayowafanya wajilimbikizie mali
tofauti na misingi iliyoachwa na hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere.
Nyerere.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment