Watu wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila mwenye umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma mwenye umri wa miaka 20 (mwanaume) ambao walitambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha,walikamatwa jana majira ya saa 12 asubuhi katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.
Kwa mujibu wa mahojiano waliyofanya na Ripota wa Blogu ya GSengo wachawi hao wanasema kuwa walipewa amri na wakuu wao wanao ishi chini ya maji kuwachukuwa watu watatu wa kanisa hilo kwa mazingira ya kichawi ili wawauwe kwaajili ya kafara na mazindiko.
Zana za Kazi za wachawi hao a.k.a wazee wa flight,ambapo mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.
Wananchi na baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi Mwanza wakiwa wamewazingira wachawi hao katika viwanja vya polisi Mwanza leo asubuhi katika kuchukuwa maelezo.
Mchungaji wa kanisa la Ufunua Diana Bandele (kushoto) na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa hilo ambao waliwakuta wachawi hao kanisani mwao majira ya saa 12 kwani muda huo ni ada kwa wao kujitakasa kwaajili ya kuianza siku ya ibada.
Ingawa jeshi la polisi linaendelea kuchunguza juu ya hali hiyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna kipengele kinacho utambua uchawi hivyo hakuna kesi inayowakabili watu hao.Picha na taarifa hii ni kwa hisani ya G Sengo Blog.
1 comments:
Wali uwawa au wako huru
Post a Comment