Tone

Tone
Home » » Utapeli wamfikisha pabaya Muunguja

Utapeli wamfikisha pabaya Muunguja

Mkazi mmoja wa Unguja, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi hati ya kumrithi isivyo halali, Mariam Masanja.
Hukumu hiyo dhidi ya Sharifa Mohamed (61), ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Soniva Mwajombe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Juma Sarige, aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa, alighushi hati hiyo ili kuchukua nyumba na magari mawili, aliyoyarithi mume wa marehemu, Faraji Ahmed (47).
Kwa upande wake, Ahmed, alidai kuwa alioana na Mariam Masanja mwaka 1996 na kufanikiwa kuwa na magari mawili, trekta moja na nyumba mbili. Alisema hata hivyo hawakufanikiwa kuwa na watoto.
Pia alisema upande wa mkewe hakuwa na ndugu wa yeyote.
Alidaiwa kuwa Novemba 2008, alikwenda Mwanza, kulipia kodi ya ardhi na jengo lakini alipewa maelezo kuwa mmiliki halali wa mali hizo ni Majid Noor Madrasat.
Alisema pia alionyeshwa barua ya urithi iliyosainiwa na katibu muhtasi Yusuph Suleiman (31) jambo ambalo lilimshtua.
Alisema baadaye alitoa taarifa polisi.
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa