Home » » MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AWASILI JIJINI MWANZA JANA JIONI KUFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA ZIWA LEO

MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AWASILI JIJINI MWANZA JANA JIONI KUFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA ZIWA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo,tayari kwa ufunguzi Kongamano la uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linaotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini,Mh. Charles Kitwanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki,wakati wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.Makamu wa Rais yupo jijini Mwanza kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linalotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika,jijini humo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali Mstaafu Fabian Massawe wakati walipotembelea hoteli ya Malaika kukagua maendeleo ya Maandalizi ya Kongamano hilo litakalofunguliwa na Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Ghalib Bilal.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki 

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa