Home » » SERIKALI CHANZO CHA MIGOMO YA WALIMU-CWT.

SERIKALI CHANZO CHA MIGOMO YA WALIMU-CWT.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

CHAMA  cha walimu  Tanzania  CWT  wilaya ya  Ukerewe, mkoani Mwanza  kimelaumu serikali  kwa kuendelea kupuuza  madai ya  walimu  hali inayosabaisha  migomo  ya mara kwa mara.
Mwenyekiti  wa  CWT  wilaya   hiyo  Pastory  Kabelinde  amewambia  wajumbe wa  mkutano  mkuu  wa chama  hicho jana  kuwa migomo ya walimu  aitasha  kama serikali  itaendelea kupuuza  madai yao.
Alisema  ni zaidi ya miaka  saba  sasa imepita  tangu  chama  hicho  kipeleke  ombi la  kupanda  mshahara wa  walimu toka  sh. 240,000 kwa mwezi  hadi  315,000 lakini  ombi hilo limepuuzwa.
Alisema  walimu  mbali ya  kupata  mshahara  usiokidhi  maitaji pia  wanafanya kazi katika  mazingira  magumu  na kuongeza kuwa  bila kutatua  matatizo ya walimu  hata  mpango wa matokeo  makubwa sasa  autafanikiwa.
Naye mwenyekiti wa  CWT  mkoa  wa Mwanza  Benedictor  Raphael  akizungumzia  matatizo  hayo  alisema   hivi sasa   kiwango cha  mshahara   kinachoweza  kukidhi  maitaji  kwa mwezi  ni sh. 700,000.
Katika  maelezo yake  alikwenda mabli  na kuwalaumu  maofisa  wa sekta  hiyo wanaosimamia   sera  kwa  kushindwa kuzingatia  taratibu zilizopo  hivyo kuwa chanzo  cha  matatizo mengi  yanayowakabili  walimu.
Akifafanua  kauri yake hiyo alisema woga na rushwa vinasababisha  maafisa hao  kusajili  shule  zisizo na sifa hivyo kusababisha walimu kupelekwa na kufanya kazi   katika mazingira  magumu.
Alisema wakati taratibu  za kusajili  shule  zipo wazi   lakini  shule  nyingi  zinakabiliwa  na  upungufu wa  majengo ikiwemo  nyumba  za walimu , mahabara, maktaba  na hata  vyoo  na madarasa.
Katibu  wa  CWT  wa  wilaya ya  Ukerewe, John  Kafimbi  amesema  hadi kufikia sasa   walimu katika wilaya hiyo wanaidai  serikali  sh. Mil.247.4  yakiwa ni madai ya  uhamisho, matibabu, mapunjo ya  mishahara , ajira mpya , likizo na  gharama za  masomo.
Alisema  walimu  katika wilaya  hiyo  wanafanya  kazi katika mazingira magumu hasa  katika  maeneo  ya visiwa vidogo  hivyo  ametaka  walaka wa maripo ya   posho  ya mazingira magumu  ualakishwe ikiwa ni pamoja   walimu hao kupewa vifaa vya  ukozi  ili wavitumie  kuokoa  maisha  yao  wakati ikitokea  ajari   majini.
Hata  hivyo  alisema  tayari  chama hicho  kimeipa serikali   muda wa  siku 60  madai  hayo yawe  tayari  yameripwa vinginevyo  kitaitisha  mgomo wa walimu.
Katibu  tawara wa wilaya  hiyo  Maliamu  Mseleche  akizungumza  baada ya  kupokea  taarifa hiyo  amewataka walimu waendelee kutimiza wajibu  wao wakati serikali ikiendelea  kutafuta ufumbuzi  wa matatizo  yao.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa