Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SAKATA la Halmahauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, kudaiwa
kupuuza na kukaidi amri iliyotolewa na serikali ya kutaka kufutwa na
kutangazwa upya zabuni ya mradi mkubwa wa maji ya bomba ya Ziwa
Victoria, wa Nyanguge-Nyambilo wilayani humo, limeanza kuchukua sura
mpya.
Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya, Jackline Liana kueleza
kushangazwa na kitendo cha Mkurugenzi wa Halmashauri, Naomi Nnko
kupuuza amri ya serikali.
Akizungumza na Tanzania Daima hivi karibuni mjini Magu kuhusiana na
tuhuma hizo, Liana alihoji sababu za mkurugenzi huyo kuruhusu kuendelea
kutekelezwa kwa mradi huo, wakati akijua serikali imezuia.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment