Mwanza. Kufuatia matukio ya uhalifu kujitokeza
mara kwa mara Kata ya Buswelu, wilayani Ilemela, mkoani Mwanza, baadhi
ya wakazi wa eneo hilo wameitaka polisi kuwajengea kituo na kuimarisha
doria.
Hivi karibuni kata hiyo imekumbwa na matukio ya
uhalifu baada ya watu wanaominika ni majambazi, kuvamia nyumba kadhaa na
maduka kisha kupora mali mbalimbali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi wa eneo
hilo walisema wamechoshwa na matukio ya uhalifu yanayojitokeza mara kwa
mara na kwamba, hivi wanataka polisi kuwajengea kituo.
Mmoja wa wakazi hao, Jackline Ismail alisema
anashangaa kitendo cha Serikali kuamua kujenga Makao Makuu ya Wilaya ya
Ilemela ndani ya kata yao bila ya kujenga kituo cha polisi.
“Hivi wanashindwa kujenga kituo cha polisi, ukizingatia watu wengi wanahamia huku wilayani?” alihoji Ismail.
Aliomba Serikali kuangalia suala la usalama wao.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walienda
mbali zaidi na kudai kwamba kituo cha polisi cha Mwatex wanachokitumia
kupata huduma kiko mbali na hivyo kupelekea wao kushindwa kupata huduma .
Vivian Mtei,Gerald Joseph pamoja na Mhoja walisema
kuwa ni muda sasa wa serikali kuhakikisha wanajenga kituo cha polisi
sanjari na kuimarisha doria ya mara kwa mara katika eneo hilo kwa lengo
la kudhibiti uhalifu .
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment