Tone

Tone
Home » » Ukerewe wasaka wakimbizi katika visiwa vidogo

Ukerewe wasaka wakimbizi katika visiwa vidogo

WILAYA ya Ukerewe imeanzisha msako kabambe katika visiwa vyake vyote kuwasaka wakimbizi haramu. Inasemekena watu hao wamekimbilia katika visiwa hivyo kukwepa operesheni kimbunga iliyofanyika katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita. Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mary Tesha ameieleza Rai kwa simu kuwa operesheni hiyo inavihusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama wilayani humo.


Aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo hivyo kuwafichua wahamiaji haramu waliokimbilia katika visiwa hivyo kukwepa mkono wa sheria.

DC Tesha alisema doria hiyo inafanyika katika visiwa vyote vya Ukerewe.

Alisema hiyo inatokana na taarifa kuwa baadhi ya wakimbizi waliokuwa wakiishi kinyemela katika mikoa iliyofanyika operesheni hiyo wamekimbilia katika baadhi ya visiwa vya Wilaya ya Ukerewe kujificha kukwepa kurejeshwa makwao.

“Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ukerewe iliketi chini yangu baada ya kupata taarifa za kuwapo wakimbizi waliokimbilia katika viswa vya Ukerewe.

“Kwa hivi sasa ninavyozungumza nawe tayari vikosi vya ulinzi na usalama viko vinafanya doria katika visiwa vya Ukerewe kuwasaka wakimbizi haramu, mwito wangu kwa wananchi ni kuhakikisha wanatoa taarifa na kuacha kuwaficha wakimbizi hao,” alisema.

Chanzo;Mtanza

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa