SERIKALI imeshauriwa kuharakisha mpango wa kujenga vyuo vya ufundi
stadi (VETA) kila wilaya nchini, ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa
nchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza,
Bonaventra Kiswaga, alitoa ushauri huo kwenye mahafali ya nane ya
wanafunzi 25 waliohitimu elimu ya Ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Mt.
Joseph Kirumba jijini Mwanza.
Kiswaga alisema upo umuhimu kwa serikali kutenga fedha za kutosha
katika kufikia malengo hayo, kwani hiyo itachangia maradufu ukuaji wa
uchumi.
“Mpango uliopo wa serikali kujenga vyuo vya ufundi stadi kila wilaya
ni mzuri katika maendeleo ya Watanzania, iwapo utatekelezwa ipasavyo.
“Kwa hiyo, naishauri serikali itumie fedha zake za ndani na zile za
wahisani kujenga vyuo vingi vya ufundi nchini, maana hiyo itaongeza
soko la ajira na kukuza uchumi wa wananchi wetu,” alisema Kiswaga.
Pia aliupongeza uongozi wa Chuo cha Ufundi Mt. Joseph kinachomilikiwa
na Kanisa Katoliki Kirumba, kwa mikakati yake ya utoaji elimu ya
ufundi stadi kwa vijana.
Kuhusu wahitimu, aliwataka vijana hao kuwa na malengo ya kujiajiri na si kuajiriwa.
Awali, akisoma risala ya chuo hicho, Mkuu wa Chuo hicho, Sister
Benisia Symphorian alisema wanakishukuru Chuo cha VETA Mwanza kwani
kimekuwa kikiwasadia vitu mbalimbali.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment