Tone

Tone
Home » » Ajabu na kweli: Mtoto azaliwa bila viungo vya uzazi, Wauguzi washindwa kujua kama ni wa kike au wa kiume

Ajabu na kweli: Mtoto azaliwa bila viungo vya uzazi, Wauguzi washindwa kujua kama ni wa kike au wa kiume




Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kisaba katika kisiwa cha maisome wilayani Sengerema Mkoani Mwanza amejifungua mtoto wa ajabu akiwa hana sehemu za siri hali ambayo imesababisha kutojulikana jinsia yake.
Mwananmke huyo anayejulikana kwa jina la Gaundesin Sebastiani (30) amejifungua kichanga hicho  juzi majira ya saa 4 asubuhi katika zahanati ya AICT Kisaba kisiwani humo.
Mama huyo anasema alianza kujisikia kuumwa tumbo majira ya asubuhi na hivyo kuamua kwenda katika zahanati hiyo kisha kijifungua kichanga hicho chenye uzito wa kilogramu 3, huku kikiwa hakina sehemu za siri kama anavyoelezea.
Kwa upande wake muuguzi wa zamu wa zahanati hiyo aliyetoa huduma kwa mzazi huyo Fidesia Marco anazungumzia mazingira ya kuzaliwa kwa kichanga hicho pamoja na taratibu za kumpeleka katika hospitali ya wilaya ya sengerema..
Diwani wa kata ya Maisome, Mazabari Mtanzania anasema tayari mzazi huyo na kichanga chake jana wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Sengerema kwa uchunguzi zaidi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa