IMEELEZWA kuwa kwa zaidi
ya miaka 23 iliyopita serikali inatumia gharama
kubwa kulinda mitiani kufuatia baadhi ya maafisa
wenye dhamana kujiusisha na wizi wa mitiani.
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe,
Mwanza Mery Tesha amesema hayo jana wakati anafungua
semina elekezi ya walimu walioteuliwa kusimamia mtiani wa
taifa wa darasa la saba mwaka huu katika wilaya hiyo.
Alisema kwa
miaka zaidi ya 23 iliyopita tangu tatizo hilo la wizi wa mitiani
limejitokeza linaendelea kughalimu fedha nyingi badala
ya kuzielekezwa katika huduma nyingine za kijamii.
Akifafanua alisema
wakati wa kipindi cha miaka ya nyuma mitiani hasa ya
elimu ya msingi, Sekondari na hata ya vyuo ilifanyika
chini ya viongozi wa ngazi hizo tofauti na ilivyo sasa.
Kufuatia hali hiyo
ameitaka jamii nzima hasa maafisa wenye dhamana
kuacha vitendo hivyo kwa sababu mbali ya kupoteza
fedaha nyingi za umma pia vinazalisha wataalumu
wasiona sifa.
Afisa elimu ya msingi wa
wilaya hiyo Fidelis Munyogwa alisema jumla ya wanafunzi
8,969 kati yao wasichana 4,508 wanatarajia
kufanya mtiani wataifa wa darasa la saba mwaka huu kukiwa na
ongezeko la wanafunzi 441 ikilinganishwa na mwaka jana.
Alieleza kuwa mwaka
uliopita wa 2012 wanafunzi 8,538 walifanya mtiani
huo huku wengine 171 sawa na asilimia 2.5
walishindwa kufanya mtiani huo kwa sababu ya utoro.
Hata hivyo alisema
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika wilaya
hiyo bado kipo chini kwasababu ya changamo nyingi
ikiwemo tatizo la wanafunzi wengi kuwa katika
chumba kimoja.

0 comments:
Post a Comment