Na George Ramadhan
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekemea imani potofu miongoni mwa jamii ya Wasukuma ya kuwaua vikongwe hususani wenye macho mekundu kwa kudhani ni wachawi.
Ametoa karipio hilo mjini Ngudu jana wakati akiwa katika ziara ya siku moja ya kutembelea wilaya ya Kwimba ambapo pamoja na mambo mengine alizindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pinda aliwataka watu wenye imani hiyo potofu kuacha nongwa kwa kudhani kila mzee mwenye macho mekundu ni mchawi.

Alisema kwa vyovyote vile mtu anapokuwa mzee anakuwa na mabadiliko mengi katika mwili wake ikiwa ni pamoja na macho kugeuka rangi na kuwa mekundu kwa sababu mbalimbali.
“Yaani mtu kuwa na macho mekundu imekuwa nongwa!” alionyesha mshangao na kuongeza “Kama hii ndio imani yenu kwamba kila mzee mwenye macho mekundu ni mchawi basi ni wazi mtaua wengi kwa sababu katika umri mkubwa lazima mtu atapata mabadiliko ikiwa ni pamoja na macho kuwa mekundu, nywele kuwa nyeupe nk.”alisema Pinda.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza kujipanga na kuhakikisha hakuna mzee yeyote atakayeuawa kwa imani za kishirikina.
Alisema Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama inapaswa kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya athari za mauaji hayo na kwamba hatua kwa hatua hatimaye mauaji ya aina hiyo yatakwisha kabisa.

Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment