Tone

Tone
Home » » CHAMA CHA TADEA KUFANYA ZIARA MKOANI MWANZA ILI KUKIIMARISHA KWA AJILI YA UCHAGUZI UJAO.

CHAMA CHA TADEA KUFANYA ZIARA MKOANI MWANZA ILI KUKIIMARISHA KWA AJILI YA UCHAGUZI UJAO.


 Viongozi wa chama cha Tadea kutoka kushoto ni Tiba Deus katibu wa Tadea Mkoa wa Mwanza, Richar Gagi Mwenyekiti wa Tadea Mkoa wa Mwanza, Juma Ally Khatibu Katibu Mkuu wa Tadea Taifa na Charles Dotto Lubala Naibu katibu Mwenezi wa Taifa wa chama cha Tadea katika mkutano na waandishi wa habari.
 Juma Ally Kahtibu Katibu wa Taifa wa chama cha Tadea akieleza kusudi la ziara ya chama cha Tadea katika Mkoa wa Kanda ya Ziwa huku waandishi wa habari.
 Hii hapa ni kadi ya uanachama ambayo katibu wa taifa wa chama cha Tadea Juma Ally Khatibu ameishikilia akiwaonya waandishi jinsi taswira yake ilivyo.
 Afisa habari wa habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Atley Kuni akiwa na Jacob Marikus wa Star Tv.
 Mwandishi Revocatus Herman wa gazeti la Baruti na Blandina Aristides wa gazeti la Uhuru wakiandika yale ya muhimu kutoka viongozi wa chama cha Tadea.
   George Ramadhan wa Gazeti la Nipashe na Dotto Emmanuel Bulendu wa Redio Saut wakisikiliza.
             Mwandishi Lonely Nzali na Mkurugenzi wa gazeti la Baruti Gerald Robert.
 Kutoka kushoto Issack Wakuganda wa Metro fm, Wilhelm Mulinda wa Majira , Zuhura Makuka wa Afya Redio, Grace Chilongola wa Habari leo na Mwandishi Albert G Sengo wa Clouds Fm wakiwa makini katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Tadea.


WATANZIA wameombwa kuwa wazalendo na kuacha ubinafsi kama alivyokuwa  Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuweza kulinda rasilmali ya nchi yetu na ya vizazi vijavyo maana baadhi ya viongozi waliopo madarakani si wazalendo na hivyo kupelekea upotevu wa rasilmali kubwa za nchi ya Tanzania. 

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha The Tanzania Democratic Alliance TADEA  Taifa Juma Ally Khatibu katika mkutano na waandishi wa habari leo kuhusu kampeni walinayo ya kuimarisha chama chao Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla ili kizidi kukubalika na kupendwa zaidi na wananchi wa rika yote.

Amesema kuwa chama cha Tadea kimejipanga kusimamisha wagombea wa ngazi za kata ishirini na saba Tanzania na kila Mgombea atatumia shilingi Millini tatu na kufanya jumla yake kuwa Milioni themanini na saba na vilevile wamejipanga kusimamisha wagombea ubunge wa Urais katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka elfu mbili na kumi na tano.

Aidha amesema kuwa Watanzania wawe makini ya baadhi ya Vyama Vya kisiasa hapa Nchini vinajuhusisha na Nchi za Kimagaribu ili kuepusha maafa ambayo yanaweza kutokea kama katika nchi za Libya, Tunisia, Misri na nyingine ambazo zimekosa amani baada ya kuruhusu machafuko kutokea nchini mwao.

Pia amewakaribisha wanasiasa wa aina zote vijana kwa wazee ambao wamefukuzwa na Vyama vyao kujiunga na chama cha Tadea ambacho mara zote kimekuwa makini toka kianzishwe.

Chama cha Tadea kimeanzishwa mwezi wa saba mwaka elfu moja mia tisa na tisini na mbili na Marehemu Oscar Kambona na kupewa usajili namba tatu, na hii ni baada ya Chama cha Mapinduzi CCM na Chama cha Wananchi CUF

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa