na Jovither Kaijage, Ukerewe
WALIMU
wanne wa Shule ya Msingi Hamkoko na msimamizi mmoja wa mitihani, wamefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa
mtihani wa taifa wa darasa la saba, huku Jeshi la Polisi likiendelea kumtafuta
mwalimu mwingine aliyetoroka.
Watuhumiwa
hao walisomewa mashtaka yanayowakabili na Mwendesha Mashtaka wa Polisi,
Inspekta Samwel Onyango mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Charles
Bilomela.
Mwendesha
Mashtaka alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda makosa
hayo Septemba 19, mwaka huu majira ya saa 5:10 asubuhi katika Shule ya Msingi
Hamkoko.
Alisema
washtakiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za makosa ya kula njama na kutenda kosa
wakiwa watumishi wa umma, wizi wa mtihani wa taifa wa darasa la saba pamoja na
kupatikana na nyaraka za serikali mali ya Baraza la Mitihani kinyume na sheria
kifungu cha 183 cha makosa ya jinai.
Kwa
mujibu wa Mwendesha Mashtaka washtakiwa hao walikamatwa nyumbani kwa Mwalimu
Kija Songoli wakiendelea na harakati za kuandaa majibu ya mtihani wa Hisabati
kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi.
Walimu
hao ni Kija Songoli (30), Jenifreda Edward (28), Mariam Kateti (26) na
Marycelina Malisel (25) na Msimamizi wa Mitihani wa Taifa wa darasa la saba,
Leonida Anthony (32).
Mwalimu
mwingine aliyetambuliwa kwa jina la Diana Shishanga anayetuhumiwa kushiriki
kutenda makosa hayo, anatafutwa na polisi ili aunganishwe na wenzake baada ya
kutoroka.
Watuhumiwa
hao walikana mashtaka na kesi hiyo itafikishwa tena mahakamani Oktoba 8, mwaka
huu. Wapo nje kwa dhamana.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment