Na Elizabeth Hombo, Dar es
Salaam
WATU watatu wanaodaiwa kuwa wavuvi, wameuawa kinyama na
wenzao kwa kukatwakatwa mapanga, baada ya kukataa kutoa nyavu za kuvulia samaki
ndani ya Ziwa Victoria.
Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Sinza Kijiweni mjini Dar es Salaam jana, ndugu wa wavuvi hao, Ramadhani Mohamed alisema, tukio hilo, lilitokea Agosti 20, mwaka huu ndani Victoria na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.
Alisema baada ya tukio hilo, alikwenda kuripoti kituo cha polisi Busisi, ambako walifanikiwa kumkamata mtu mmoja, lakini walimwachia katika mazingira ya kutatanisha.
“Tunasikitika kuona mtu anakamatwa kwa makosa makubwa kama haya, lakini akaachiwa katika mazingira ya kutatanisha… naomba vyombo vya dola vinisaidie,” alisema Mohamed, …baada ya kupita siku tano, nilipigiwa simu kuwa wenzangu wanashangaa kutoonekana, ndipo nikapigiwa simu kuwa, akina Mathayo.
“Siku iliyofuata kuna jamaa mmoja akapeleka baiskeli ya kina Mathayo nyumbani, kwa sababu walikuwa kila wanapoenda kuvua samaki, wanaacha baiskeli kwa jamaa mmoja jirani na pale ziwani,” alisema.
Polisi wakiongozana na kaka zangu, wengine wakaenda ziwani na wakakuta vipande vya vichwa, mikono, miguu na sehemu za siri zikiwa zimetengana,” alisema.
Aliwataja marehemu kuwa ni Mathayo Kulwa (36), Vumilia Kulwa (34), mwingine hakufahamika kwa jina kwa kuwa alikuwa ni marafiki tu na ndugu zake wote ni wakazi wa kijijini cha Nyamasale.
Alisema baada ya polisi kufanya uchunguzi, walifanikiwa kumkamata mtu mmoja, ambaye baadaye aliachiwa.
Akizungumza na MTANZANIA, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Sengerema, Pudensia Protas alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba hatua za kuwasaka wahusika zinaendelea.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba ameagiza jeshi hilo wilayani Sengerema, kufanya uchunguzi wa tukio hilo na apewe taarifa ndani ya siku tatu.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment