AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
leo amepokea magari hamsini ya kubebea wagonjwa pamoja na magari 8 ya
kuratibu shughuli za huduma za afya ya mama na mtoto yenye thamani ya
shilingi bilioni 5.9 ambayo yamekabidhiwa kwa Wabunge wa Mikoa ya
Kanda ya Ziwa ikiwemo Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kigoma
Waziri
Ummy amelishukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) na UNFPA kwa kuendelea
kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili
watanzania, ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.
Alizitaja
changamoto zilizoonekana katika mikoa hiyo ni huduma hafifu ya rufaa
kwa wanawake wajawazito kwa kukosa magari ya kubebea wagonjwa, ukosefu
wa damu salama, ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya
mama ikiwemo kutotambua dalili hatari za wakati wa ujauzito pamoja na
baadhi ya watumishi wasiokuwa na stadi za kuokoa maisha ambayo
yanachangia wingi wa vifo vitokanavyo na uzazi
Tafiti
zilizofanyika mwaka 2010 na tathmini iliyofanyika mwaka 2015 wakati wa
kuandaa mpango kazi wa matokeo makubwa sasa, Mikoa ya Kanda ya Ziwa
ikiwemo Kigoma ilionekana kuwa na viashiria hafifu vya afya ya mama na
mtoto kwa mfano; utumiaji mdogo wa uzazi wa mpango, wanawake wachache
wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya pamoja na vifo
vingi vitokanavyo na uzazi.
Wizara
ya Afya imekua ikifanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana na
tatizo hilo ambapo kwa awamu hii ya tano tumetengeneza mpango mmoja
utakaohusika na masuala ya uzazi wa afya ya mama na watoto na vijana
ambapo ndani ya miaka minne hadi kufikia mwaka 2020 tuwe tumepunguza
vifo vya akina mama wajawazito kutoka 432 hadi 292 kutoka kila kizazi
hai laki moja na kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano Tanzania
imefanikiwa kufikia lengo namba nne la malengo ya maendeleo ya milenia
kwa kupunguza vifo kutoka 50 hadi 40 katika vizazi hai 1,000.
Aidha
Waziri Ummy amewataka Wabunge, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Wilaya
kuyatumia magari hayo ipasavyo yaani, kwa shughuli iliyokusudiwa,
vilevile kuyakatia bima ya ajali pamoja na kuiomba jamii, Taasisi zisizo
za kiserikali kuunganisha nguvu kwani vifo vitokananyo na uzazi
vinazuilika.
IMETOLEWA NA
Nsachris Mwamwaja
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-AFYA
14/12/2016
0 comments:
Post a Comment