Home » » SHIRIKA LA TAYOA LASAIDIA KUONGEZA UELEWA KUHUSU SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI MKOANI MWANZA.

SHIRIKA LA TAYOA LASAIDIA KUONGEZA UELEWA KUHUSU SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI MKOANI MWANZA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya afya pamoja na ukatili wa kijinsia kwa vijana na wanawake nchini la Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.
#BMGHabari
Wadau wa afya mkoani Mwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.
Mratibu wa Afya ya Uzazi ngazi ya jamii mkoani Mwanza, Esperance Makuza, akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi ngazi ya mkoa wa Mwanza.
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, akifafanua namna mradi huo ulivyofanya kazi, mafanikio na changamoto zake.
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, akifafanua namna mradi huo ulivyofanya kazi, mafanikio na changamoto zake.
Baadhi ya wadau wa afya mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi 
Baadhi ya wanahabari pamoja na wadau wa afya mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi 
Mmoja wa watumishi wa afya mkoani Mwanza
Mradi huo ulifadhiriwa na Pink Ribbon Red Ribbon pamoja na washirika wengine kama wanavyoonekana katika picha. Mitandao ya simu ilisaidia kutoa nambari za bure ambazo ni 117 kwa ajili ya wananchi kupiga ili kuelimishwa kuhusu Saratani.

Uelewa kuhusu dalili za awali za maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake mkoani Mwanza, umeongezeka na hivyo kufanya idadi ya wanawake wanaojitokeza kupima maambukizi hayo kufikia wanawake 60 kwa mwezi.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ikiwemo TAYOA katika kuhakikisha akina mama nchini wanafahamu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa awali kuhusu maambukizi ya saratani kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.

Katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwezi April mwaka 2014, zaidi ya akina mama elfu 20 mkoani Mwanza wamefikiwa na kupewa elimu kuhusiana na saratani ya shingo ya kizazi, kuwaongezea ujuzi watoa huduma za afya wapatao 70 katika ngazi za jamii pamoja na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya uchunguzi wa dalili za awali za saratani hiyo katika vituo vya afya mkoani Mwanza ambapo tamati ya mradi huo ni Disemba 31 mwaka huu.

Aidha mradi huo umesaidia kuwasafirisha akinamama 392 mkoani Mwanza, kwenda katika hospitali za rufaa ikiwemo Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa Saratani ya shingo ya kizazi ambapo miongoni mwao zaidi ya akina mama 70 wamepatiwa matibabu.

Awali Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, amebainisha kwamba wakati mradi huo unaanza kulikuwa na dhana potofu kuhusiana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambayo wanawake wengi walikuwa wakiamini wamerogwa na hivyo kuchelewa kufika hospitalini huku baadhi yao wakikimbiwa na waume zao.

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi mkoani Mwanza, Mratibu wa Afya ya Uzazi ngazi ya jamii, Esperance Makuza, amewahimiza watoa huduma wa afya walionufaika na mafunzo yaliyotolewa katika mradi huo, kuyatumia mafunzo hayo kutoa huduma zinayostahili ili kuwanusuru akina mama na madhara yatokanayo na saratani hiyo.

Inaelezwa kwamba zaidi ya asilimia 80 ya akina mama wanaougua saratani ya shingo ya kizazi nchini hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kufanya uchunguzi na kupatiwa tiba mapema, ikizingatiwa kwamba saratani hiyo hutibiwa ikiwa mgonjwa atawahi matibabu.

Aidha akina mama wanakumbushwa kuzingatia kanuni bora za kiafya ikiwemo kufanya mazoezi, kujiepusha na uvutaji wa sigara, ulevi pamoja na wapenzi wengi ili kuondokana na maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa