Naibu Waziri wa
Kilimo, Mifugo na UvuviMhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhamishia Bodi ya Pamba katika
Mkoa wa Mwanza kabla ya Novemba 10 mwaka huu ili kuhakikisha wakulima wa
pamba waliopo katika mkoa huo wanapata huduma zilizo bora kwa ukaribu
na haraka.
Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. William
Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto Biteko
lililohoji juu ya hatua ya Serikali kwa wakulima walioathirika na
pembejeo zilizotolewa ambazo hazikuwa na ubora pamoja na kuhamishia Bodi
ya Pamba katika mkoa huo.
”ili
kuwafikia kirahisi wakulima wa pamba waliopo mkoani Mwanza, Wizara
imeamua kuhamishia Bodi hiyo katika mkoa huo na kwa taarifa zilizopo
Bodi hiyo inatakiwa kuhama haraka iwezekanavyo kabla ya Novemba 10 mwaka
huu”, alisema Mhe.Ole Nasha.
Kwa
upande wa matatizo ya pembejeo, Mhe. Ole Nasha amesema kuwa Serikali
tayari ina taarifa kuhusu tatizo lililowapata wakulima wa pamba katika
maeneo mbalimbali kwa kusambaziwa viuatilifu pamoja na mbegu ambazo
hazikuwa na ubora unaotakiwa hivyo kuathiri wakulima nchini.
“Serikali
iliiagiza Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) kufanya
uchunguzi wa malalamiko ya wakulima ambao ulibaini kuwa viuatilifu hivyo
vilikuwa na utendaji hafifu hivyo Serikali itaanza kuzalisha mbegu bora
za pamba za UK08 ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena”, alisema
Mhe. Ole Nasha.
Naibu
Waziri huyo amefafanua kuwa kufuatia changamoto hizo za uotaji wa
mbegu, Serikali iliamua kufanya majaribio ya utoaji wa mbegu ambazo
zilikuwa zikisambazwa hapo awali bila kujua ufanisi katika uotaji wake.
Amethibitisha
kuwa, matokeo ya jaribio hilo yamewezesha kutoa maelekezo kuhusu aina
za mbegu za pamba zenye sifa za msingi ambazo zitasambazwa kwa wakulima
katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017.
0 comments:
Post a Comment