SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
ZAIDI YA VIBANDA 400 VINAVYOTUMIWA
KAMA MAKAZI YA WAVUVI PINDI WANAPOKUWA KATIKA SHUGHULI YA UVUVI
VIMETEKETEA KWA MOTO WILAYANI SENGEREMA.WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA NA BHANGI KATIKA WILAYA YA NYAMAGANA NA ILEMELA
KWAMBA TAREHE 20.06.2016 MAJIRA YA
SAA 18:30HRS JIONI KATIKA ENEO LA MCHANGANI KIJIJI NA KATA YA BUHAMA
TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ZAIDI YA VIBANDA
400 VINAVYOTUMIWA KAMA MAKAZI YA WAVUVI PINDI WANAPOKUWA KATIKA SHUGHULI
YA UVUVI VIMETEKETEKEA KWA MOTO NA KUPELEKEA HASARA YA VITU NA MALI
ZILIKUEPO NDANI YA VIBANDA HIVYO.
INADAIWA KUWA MOTO HUO ULIWASHWA
NA MVUVI ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA FRANK MKAZI WA ENEO HILO LA
VIBANDA VYA MCHANGANI ALIYEWASHA MOTO KWA AJILI YA KUCHOMA UTITIRI
KWENYE KIBANDA CHAKE KILICHO TENGENEZWA KWA MABANZI NA NYASI KISHA MOTO
HUO KULIPUKA NA KUSAMBAA KATIKA VIBANDA VINGINE.
AIDHA INASEMEKANA KUWA MOTO HUO
ULIWEZA KUSAMBAA KWA HARAKA KATIKA VIBANDA HIVYO, KUTOKANA NA VIBANDA
HIVYO KUTENGENEZWA KWA NYASI NA SANDARUSI HALI ILIYOPELEKEA WATU
KUSHINDWA KUUZIMA NA KUTEKETEZA MALI ZA WAVUVI HAO.
THAMANI YA MALI NA VITU AMBAVYO
VIMETEKETEA KWA MOTO HUO BADO HAIJAFAHAMIKA, MTUHUMIWA WA TUKIO HILO
AMETOROKA, JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA JITIHADA ZA KUMSAKA NA KUWEZA
KUMTIA NGUVUNI MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU, LAKINI PIA UCHUNGUZI NA
UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUJITAHIDI KUTENGENEZA NA
KUJENGA MAKAZI SALAMA AMBAYO YATAWEZA KUZUI KUTOKEA KWA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MNAMO TAREHE 21.06.2016 MAJIRA YA
SAA 14:00HRS MCHANA KATIKA ENEO LA NYASAKA WILAYANI ILEMELA JIJI NA MKOA
WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO PAMOJA NA DORIA WALIFANIKIWA
KUMKAMATA HASSAN SALUM MIAKA [32] MKAZI WA NYASAKA AKIWA NA MADAWA YA
KULEVYA AINA YA BHANGI KILO 100 KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA
NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA INADAIWA KUWA MTUHUMIWA
ANAJIHUSISHA KATIKA BIASHARA HIYO KWA MUDA MREFU KATIKA MAENEO HAYO
TAJWA HAPO JUU AKISHIRIKIANA NA WENZAKE, NDIPO JESHI LA POLISI LILIWEZA
KUPOKEA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA NA KUWEZA KUMTIA NGUVUNI MTUHUMIWA
TAJWA HAPO JUU.
KATIKA TUKIO LINGINE WAKATI ASKARI
WANAENDELEA NA MISAKO MAJIRA YA SAA 14:30 KATIKA ENEO LA NYAKATO NUNDU
WILAYANI NYAMAGANA, ASKARI WALIWEZA KUMKAMATA MESHACK NICOLAUS MIAKA 26
MKAZI WA NYAKATO AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI KILO 100
KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA
AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUJIHUSISHA NA UVUTAJI PAMOJA NA BIASHARA YA
BHANGI KATIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU, NDIPO JESHI LA POLISI LILIWEZA
KUPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NA KUFANIKIWA KUMKAMATA.
WATUHUMIWA WOTE WAWILI WAPO CHINI
YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WA
KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA YAKIENDELEA, JESHI LA POLISI
LINAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA MTANDAO WA
WATU WANAOSHIRIKIANA NA WAHALIFU HAO KATIKA UTEKELEZAJI BIASHARA HIYO YA
MADAWA YA KULEVYA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WAWILI
WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
VIJANA WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA
NA BIASHARA HARUMU YA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO YATAWALETEA MATATIZO NA
KUSHINDWA KULILETEA TAIFA MAENDELEO, NA KATIKA HILO JESHI LA POLISI
LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA LINAWATIA NGUVUNI WALE WOTE
WANAOJIHUSHISHA NA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA YA AINA ZOTE.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
0 comments:
Post a Comment