Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Padri Privatus Karugendo
Kwa ufupi
Huyu aliandika akitetea hoja yake kwa takwimu, hata
waliomfuatia nao walimjibu kwa takwimu. Hivyo hawa wote hawawezi kuwa
wapumbavu kwa wanayoyaamini.
Hivi karibuni, mwandishi mmoja aliandika akihoji hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuwateua Waislamu kushika wizara nyeti zote.
Huyu aliandika akitetea hoja yake kwa takwimu,
hata waliomfuatia nao walimjibu kwa takwimu. Hivyo hawa wote hawawezi
kuwa wapumbavu kwa wanayoyaamini.
Ni vigumu kusema ni upumbavu au siyo upumbavu kila
mtu kushikilia hoja yake. Inategemea mtu analiangalia hili kutoka kona
ipi na kwa lengo lipi.
Kwa maoni yangu mimi, tatizo lenyewe ni kubwa
zaidi ya ndugu hawa wote wanavyoliona. Nina imani kwamba hawa watatu
waliojitokeza kuliongelea suala la udini katika Serikali wana wafuasi
wao.
Wote wanatoa ushahidi kwamba jambo hili
linaongelewa mitaani. Ni kweli linaongelewa, lakini ukweli ni kwamba
jambo ni zaidi ya Ukristo na Uislamu.
Hata kama Rais Kikwete, angejitahidi kulinganisha
uteuzi wa Wakristo na Waislamu, bado Wahaya wangekuja juu kwamba
Wanyakyusa ni wengi zaidi katika Serikali yake.
Angejaribu kutoa haki sawa kwa makabila yote, bado
watu warefu wangelalamika kwamba watu wafupi wamependelewa zaidi! Kama
angefanikiwa kutoa haki sawa kwa warefu na wafupi, basi suala la sura
lingejitokeza.
Wenye sura “nzuri” wangelalamika kwamba,
amewapendelea watu wenye sura “mbaya” Kama tunakumbuka wakati wa kampeni
kuna baadhi ya watu walikuwa wanasema kwamba mgombea Jakaya Kikwete,
alikuwa na sura ya kuvutia kuliko wagombea wengine.
Walimpenda siyo kwa sababu nyingine, ni kwa vile sura yake ni nzuri! Hivyo na sura inaweza kuwa hoja!
Tuliangalie kwa upana zaidi
Hoja yangu ni kwamba hili la kuwapendelea Waislamu
au Serikali za awamu nyingine kuwapendelea Wakristo, linakwenda mbali
zaidi ya Ukristo. Ni lazima kuliangalia kwa upana zaidi.
Malalamiko haya yanayojitokeza na ambayo
yataendelea kujitokeza kila mara ni ushahidi wa kutosha kwamba bado
hatujafanikiwa kuwa na mfumo wa kutusaidia kulenga pamoja kama Taifa
0 comments:
Post a Comment