Home » » KOMREDI KINANA ALAKIWA KWA SHAMRA SHAMRA ZA SUNGUSUNGU JIMBO LA KWIMBA

KOMREDI KINANA ALAKIWA KWA SHAMRA SHAMRA ZA SUNGUSUNGU JIMBO LA KWIMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Kikundi cha Ulinzi wa Jadi cha Sungusungu, alipowasili  katika Kijiji cha Hungumalwa njaia panda ya Mwamashinga alipoanza ziara Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Komredi Kinana akivishwa kofia ya jadi ya Sungusungu wakati wa mapokezi wilayani Kwimba.
 Komredi Kinana akipuliza filimbi mara baada ya kuvishwa mavazi ya asili wakati wa mapokezi wilayani Kwimba leo

 Komredi Kinana akiwaongoza Sungusungu mara baada ya kulakiwa na wananchi katika Kijiji cha Hungumalwa.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor akielezea mbele ya Komredi Kinana jinsi alivyosaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
 Komredi Kinana akiangalia ngoma iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa kukaguaujenzi wa  mradi wa Zahanati katika Kijiji cha Hungumalwa, katika Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor akishiriki ujenzi wa Zahanati ya Hungumalwa iliyokaguliwa na  Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana
 Wananchi mjini Ngudu, Kwimba wakimlaki Komredi Kinana huku wakiwa na bando na kumsifu mbunge wao Shanif Mansoor.
 Wananchi wakimlaki Komredi Kinana alipofika kushiriki uoandani wa miche ya miti ya Kikundi cha wajasiriamali mjini Ngudu, Kwimba leo.
 Komredi Kinana akishiriki kupanda miche ya miti katika kikundi hicho kilichopo mjini Ngudu, wilayani Kwimba.
 Komredi Kinana akifungulia maji alipofika kukagua ukamilishwaji wa ujenziwa mradi huo eneo la Majengo Mapya, mjini Ngudu, wilayani Kwimba leo.
 Mmoja wa akina mama wa Majengo Mapya mjini Ngudu, katika Jimbo la Kwimba akitwishwa ndoo ya maji na Komredi Kinana baada ya kuufungua mradi huo.
 Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor akisaidfia kumtwisha ndoo ya maji baada ya Komredi Kinana kuufungua mradi wa maji eneo la Majengo Mapya, mjini Ngudu wilayani Kwimba.
 Wauguzi n madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Ngudu wakisalimiana na Komredi Kinana aliyekwenda kukagua jengo la wagonjwa mahututi (ICU),  wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza leo.
 Komredi Kinana akisalimiana na Balozi Specioza Balele wa CCM Shina namba 12, alipomtembelea wakati wa ziara yake Jimbo la Kwimba katika Mji wa Ngudu.

 Kikundi cha Ulinzi wa Jadi cha Sungusungu kikitumbuiza kwa ngoma ya asili wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akihutubia katika mkutano huo wa hadhara .
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba, ambapo aliitaka jamii wakiwemo mabalozi wa mashina kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), ili kuepusha mauaji dhidi yao.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, ambapo alikemea tabia ya wapinzania kuwahadaa vijana nchini kuwa wakiingia madarakani wataweza kuwatekelezea kila kitu.

Aliwataka vijana wa kitanzania kuacha kabisa kuhadaika na watu wao walio waita waongo, bali wachape kazi ili kujipatia riziki zao kila siku/
 Komredi Kinana akiwapokea waliovihama vya vya upinzania na kujiunga na CCM kaatika mkutano huo wa hadhara.
 Komredi Kinana akionesha baahai ya kadi za wapinzani walioamua kuhamia CCM.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema katika Kijiji cha wilayani Kwimba akizungumza baada ya kuamua kukihama chama hicho na kuijunga na CCM wakati wa mkutano huo.
 Kinana akikabidhi msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu Mjini Ngudu. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor.
Komredi Kinana akiwa na Mbunge was Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor baada ya kukabidhi msaada wa vyereheni kwa vikundi vya akina mama wa Jimbo la Kwimba.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa