Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ameamuru maafisa watendaji wawili,
akiwemo wa kata ya Sangabuye katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela
wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 40
zilizotokana na mauzo ya viwanja vya biashara na makazi katika kijiji
cha Sangabuye kuwekwa mahabasu wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea
kufanyika.
Maofisa watendaji waliokamatwa na polisi wakati wa mkutano wa
hadhara ulioitishwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo baada ya
kulalamikiwa na wakazi wa kijiji cha kayenze kwa ubadhirifu wa shilingi
milioni 43 ni afisa mtendaji wa mtaa wa kayenze Musa Zablon Bujiku
pamoja na aliyekuwa afisa mtendaji wa kata ya Sangabuye Damas
Ntenganija. Kwa sasa Ntenganija hana kituo maalum cha kazi baada
kushushwa madaraka hadi kubakia afisa mtendaji wa mtaa- hata hivyo
hajapangiwa rasmi kituo cha kazi.
Kabla ya mkuu wa mkoa kumuagiza Ocd wa wilaya ya Ilemela kuwatia
mbaroni viongozi hao, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kayenze
waliwasilisha malalamiko ya kutafunwa kwa fedha hizo, ambapo shilingi
milioni tano zilikuwa ni kwa ajili ya uendeshaji wa mradi wa maji kwa
kuiomba serikali kuwawajibisha viongozi waliohusika na ubadhirifu huo.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza pia amesema serikali haitarudi nyuma
katika kukabiliana na uharamia unaofanyika ndani ya ziwa Victoria.
Chanzo:ITV Tanzania
kiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment