Kuna mambo mengi yanakwaza maendeleo ya michezo nchini, hususani
soka. Kama itakulazimu kuyaorodhesha mambo hayo, fursa hiyo
itakugharimu muda mrefu.
Kati ya mambo hayo, baadhi tunajitakia wenyewe.
Bado tuko kwenye utumwa wa giza nene la mfumo wa uendeshaji michezo
mchini, ambao hautoi fursa ya kuwekeza katika kuandaa vijana.
Programu nyingi za kukuza michezo nchini ni za muda mfupi, tunafikiria kuwekeza ndani ya muda mfupi na kupata mafanikio.
Kuna mifano mingi. Wenzetu waliofanikiwa kusonga
mbele katika michezo, wameweza kwa sababu ya uthubutu wa kuwekeza
kuanzia ngazi za chini. Sisi bado tuko kwenye mfumo wa maji mara moja.
Bado tunafikiria kuingiza fedha leo na kupata mafanikio siku inayofuta.
Hili ndilo tatizo letu kubwa linaloonekana kukosa tiba.
Mifumo yetu ya kukuza soka imeingiliwa na mambo ya
siasa. Viongozi wamegeuka kuwa alama ya siasa katika soka. Hili ni
tatizo lingine kubwa katika maendeleo ya soka nchini.
Kuna maswali mengi unaweza kujiuliza na usiwe na
majibu ya kutosha. Inakuaje viongozi waliopewa dhamana ya kukuza soka,
leo wanaacha majukumu hayo na kuingiza siasa?
Hivi kweli katika masuala yanayohitaji utalaamu,
tuna sababu gani ya kuingiza mambo ya siasa? Viongozi wetu wamekuwa
wepesi wa kutoa
majibu mapesi kwenye maswali magumu.
Madhara ya kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu
tunaendelea kuyashuhudia. Tanzania sasa imekuwa kama kituo cha kutimua
hovyo makocha, hii ina athari kubwa sana kwa mtazamo wa baadaye wa soka
letu.
Sina maana kocha anapokosea hapaswi kutuchukuliwa
hatua, hapana, lakini kinachoonekana ni kwamba, viongozi wetu wanaingiza
siasa zaidi kwenye michezo. Kocha anapimwaje kwa kigezo cha mechi
moja?.
Katika siasa hizo hizo, leo kuna klabu inamwajili
kocha na kumpa mkataba wa miezi sita, afanye nini? Timu gani inajengwa
na kupata mafanikio ndani ya miezi sita?
Ndiyo maana nilisema, uwezo wetu ni wa maji mara
moja. Tunataka kocha akianza kufundisha timu leo, basi apate ushindi
kila mechi na kinyume chake hafai, anatimuliwa. Tunadhani ushindi wa
timu ni kocha tu. Tunawatunza vipi wachezaji, tunawapa kwa muda
unaotakiwa mahitaji wanayostahili? Kwa nini viongozi wetu wanaingilia
utendaji wa kocha kama mwanataaluma?
Twende mbali zaidi. Nashawishika kuamini kuwa Serikali bado haijawekeza vya kutosha katika michezo. Kila mwaka bajeti ya Serikali haiipi kipaumbele cha kutosha michezo. Michezo haionekani kuwa na tija, tunaiona ni burudani tu. Michezo siyo burudani tu kama ilivyokuwa zamani. Michezo ni ajira ya kutosha kwa vijana. Dunia inabadilika kila siku, tunategemea kuona watu pia wakibadilika. Mtu asiyekubali kwenda na mabadiliko yanayoikumba dunia, ni wazi ana tatizo. Ndicho nachokiona kwenye sekta ya michezo nchini.
Chanzo:Mwananchi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment