Mwenyekiti wa kikundi cha Nuru cha wilayani Sengerema mkoani Mwanza Bw. George Tumbo akitoa utangulizi wa katika katika hafla ya kutoa msaada kwa watoto yatima iliyofanyika kwenye kituo cha Sengerema Telecentre.
Na Daniel Makaka, Sengerema
Kikundi cha Nuru group kilichopo kata ya Ibisabageni wilayani Sengerema mkoa Mwanza kimetoa msaada wa Sare za shule, viatu, Kalamu na Madaftari kwa watoto yatima 30 pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kuendelea masomo mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kikundi Bw. George Tumbo alipokuwa akiongea wa waandishi wa habari mara tu lilipomalizika zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo kwa watoto hao ambapo zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mjini Sengerema.
Alisema kuwa vifaa hivyo walivyogawa vilichukuwa thamani ya shilingi Million moja laki nane na mia tano kwa lengo la kusaidia watoto hao ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu baada ya kufiwa na wazazi wao na wengine kutelekezwa na familia zao kutokana na ugumu wa maisha.
Mtendaji wa kata ya Isabageni wilayani Sengerema Bw. Japhet Mashara akikabidhi msaada huo kwa mmoja wa wanafunzi hao.
Bw. Tumbo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho mwaka 2009 kikundi kilianza kutoa msaada kwa watoto hao mwaka 2010 wapatao 170 ambapo hadi sasa ndiyo wanaopata msaada huo wengine wakiwa shule za sekondari.
Aidha alisema kuwa baada ya kuona idadi hiyo ikiongezeka ya watoto hao kikundi kimeanzisha mpango wa kuwasaidia watoto hao kwa makundi ili wote wawezekupata huduma hiyo inayotolewa na kikundi hicho kwa lengo la kuwa saidia.
Ameongeza kuwa anaomba vikundi vingine vijitokeze kusaidia kundi la watoto kama hao ambapo wamekuwa wengi katika maeneo mbalimabli hapa nchini ili waweze kuwajengea msingi bora katika maisha.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Kikundi cha Nuru katika picha na watoto yatima waliopatiwa msaada huo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment