Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza kwa mara nyingine tena,
wameendelea kuonja adha ya migomo, ambapo leo hii wafanyabiashara zaidi
ya 600 wenye maduka makubwa na ya kati yaliyopo katika mitaa mbalimbali
ya jiji hilo wameamua kufunga maduka yao na kuisababishia serikali
hasara ya mamilioni ya shilingi.
Mgomo huo wa maduka ambao ulitangazwa kufanyika februari 11 mwaka
huu na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara Mwanza ni hatua ya
kumuunga mkono mwenyekiti wa jumuiya hiyo Tanzania Johnson Minja
anayekabiliwa na kesi katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma.
Huduma za kibiashara katika jiji la Mwanza zilionekana kuzorota
huku baadhi ya mitaa iliyozoeleka kwa pilikapilika za wananchi kufanya
manunuzi ikiwa tulivu ambapo baadhi ya wafanyabiashara niliozungumza nao
kuhusiana na mgomo huo wamelalamikia hali hiyo.
Pamoja na kuwepo kwa mgomo huo, nimeshuhudia baadhi ya maduka
kadhaa katika mtaa wa Uhuru na Liberty yakiendelea kutoa huduma, huku
wengine wakilalamikia usumbufu uliojitokeza kutokana na kusafiri umbali
mrefu kutoka katika visiwa vya wilaya ya Sengerema kuja Mwanza kutafuta
mahitaji.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment