Tone

Tone
Home » » NGELEJA ATETEA UBUNGE WA ZITTO

NGELEJA ATETEA UBUNGE WA ZITTO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Sengerema,William Ngeleja.
 
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (pichani), amesema Zitto Kabwe, bado ni mbunge halali wa Jimbo la Kigoma Kaskazini licha ya kubatizwa jina kuwa ni mbunge wa mahakama.
Alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za baadhi ya wananchi jimboni kwake waliotaka kufahamu iwapo Zitto bado ni mbunge kutokana na baadhi ya wafuasi wa Chadema kudai kutomtambua.

“Mimi siyo msemaji wa Chadema, lakini nazungumza kama mbunge wenu ili kuwaondolea mkanganyiko mlio nao ni kuwa Kabwe (Zitto) bado mbunge na ataendelea kuwa mbunge hadi mahakama itakapokuwa imetoa maelekezo mengine,” alisema Ngeleja na kushangiliwa na umati wa watu waliofurika katika mkutano huo.

Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji cha Nyantakubwa, Kata ya Kasungamile, ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku 10 ya kutembelea jimbo lake kwa lengo la kusikiliza kero na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Ngeleja, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, aliwatahadharisha wapigakura wake kuwa makini na uzushi wa kila kinachozungumzwa kuepuka kupotoshwa na inapobidi kuuliza ili kupata jibu sahihi kama walivyofanya, kwa vile hiyo ni sehemu ya wajibu wake.

Wakati wa ziara yake juzi akiwapo katika Kitongoji cha Igalagalilo, Kijiji cha Chamabanda, Kata ya Katunguru, ambako alipokewa kwa maandamano makubwa. Wakati wa mkutano, baadhi ya wajumbe walithubutu kuimba “Rais mtarajiwa” bila kutafuna maneno wakimuita “jembe lao”.

Tayari amefanya ziara katika Kata za Nyamatongo, Busisi, Nyamazugo, Nyampulukano, Chifunfu na Kasenyi, ambako alifanya mikutano ya hadhara, huku baadhi wakidai kukerwa na baadhi ya wanachama kuanza kupitapita wakifanya kampeni za ubunge kabla ya muda.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa