Home » » BENKI YA KBC YAKABIDHI MASHINE KUPIMIA WAJAWZITO

BENKI YA KBC YAKABIDHI MASHINE KUPIMIA WAJAWZITO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
KITUO cha Afya cha Makongoro, jijini hapa kimepokea msaada wa mashine ya Ultra Sound na Suction zenye thamani ya Sh milioni 15 kwa ajili ya kupimia wajawazito na wagonjwa wengine.
Msaada huo ulikabidhiwa jana na Meneja wa Benki ya KCB, tawi la Mwanza, Joseph Njile kwenye hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo.
“Ni matumaini ya KCB kuwa uongozi wa Kituo cha Makongoro utavitunza vifaa hivyo ili vidumu na kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi jijini hapa,” alisema.
Alisema benki hiyo imekuwa na kawaida ya kutembelea vituo ambavyo imevipatia misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada husika.
Alisema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2011 hadi 2014, benki ya KCB imetoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya taasisi za Mwanza vyenye thamani ya Sh milioni 80.
Mwaka jana benki ya KCB ilitoa misaada kitaifa yenye jumla ya thamani ya Sh milioni 300 wakati mwaka huu bajeti yao ni Sh milioni 350 kwa ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka kwenye mikoa ya Arusha, Moshi, Morogoro, Zanzibar na Dar es Salaam.
Kwa upande wake Kaimu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Dismas Masumu aliishukuru benki ya KCB kwa msaada waliowapatia huku akiomba misaada zaidi katika nyanja ya elimu.
Chanzo:Habari Leo

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa