Tone

Tone
Home » » Taasisi ya Kivulini yaanza vikao vya utendaji kazi kwa wasaidizi wa kisheria wilaya za mkoani Mwanza

Taasisi ya Kivulini yaanza vikao vya utendaji kazi kwa wasaidizi wa kisheria wilaya za mkoani Mwanza

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

1
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Masele akizungumza na Wasaidizi wa Kisheria (hawapo pichani) wilaya ya Sengerema cha tathmini ya utendaji kazi wa Wasaidizi wa kisheria chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki za binadamu kilichoanza mapema jana asubuhi.
Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kutetea haki za Wanawake, KIVULINI, yenye makao makuu jijini Mwanza imeanza kufanya vikao vya tathmini ya utendeji kazi wa wasaidizi wa kisheria kwa robo mwaka ya pili katika ngazi za wilaya chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu.
Vikao hivyo vilivyoanza leo katika wilaya ya Sengerema kwa kukutana na wasaidizi wa kisheria 25 wanaofanya kazi ya kutatua migogoro ya kisheria katika vijiniwilaya ya sengerema huku vikao hovyo vinatarajiwa kufanyika pia katika wilaya ya Magu, Misungwi na Kwimba zote zipo ndani ya mkoa wa Mwanza.
Kivulini kupitia mradi wa msaada wa kisheria imetekeleza shughuli mbalimbali kwa lengo la kuisaidia jamii kupata uelewa wa haki zao za kisheria na pia kundeleza uwepo wa elimu na ushauri wa kisheria katika maeneo ambayo mradi unatekelezwa.
Na juhudi kubwa imewekwa katika kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria kwasabaabu wasidizi wa kisheria wanaitajika ili kuiwezesha jamii kuweza kupata haki hasa wale walioko pembezoni.Na kwa kupitia umoja wa wasaidizi wa kisheria wataweza kutoa elimu kwa wanajamii ili waweze kujua haki zo za kisheria .na matatizo yanayopelekea uvunjifu wa haki na kuchukua hatua.
2
Kivulini Iliwezesha uundwaji wa umoja wa vikundi vinne vya  wasaidizi wa kisheria ktika wilaya ya kwimba,Misungwi,Sengerema,Na Magu  na umoja huo unaundwa na jumla ya wajumbe 25 kila kikundi ambao walipata mafunzo ya wasaidizi wa kisheria kwa kutumia mtaala wa chama cha wanasheria Tanganyika.
Wasaidizi wa kisheria wameendelea kutoa huduma ya ushauri wa kisheria kwa wanajamii  hasa kwa makundi yasiyojiweza katika kata 52, kwa kipindi cha robo mwaka ya pili wasaidizi wa kisheria wamepokea mashauri 129 kwa ujumla katika mashauri hayo yaliyokamilika ni mashauri 60 yaliyotolewa rufaa ni 43 na yanayoendelea nimashauri 43, ukilinganisha na robo mwaka ya kwanza ambapo mashauri 200 yalipokelewa ambayo inafanya jumla ya mashauri 329 yaliyopokelewa na wasaidizi wa kisheria.
3
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria katika wilaya ya Sengerema wakiwa katika kikao cha tathmini ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha robo ya pili ya Mwaka kwa mradi wa  mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu.
4
Bi Eunice Mayengela Mwanasheria toka Shirika la KIVULINI akitoa ripoti ya utendaji kazi wa Mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu kwa washiriki. Bi. Eunice alisema kuwa Lengo la umoja wa Wasaidizi wa kisheria ni kuhakikisha unasimamia shuguli zote za msaada wa kisheria katika wilaya husika, na ni kiunganishi cha wasidizi wa kisheria katika ngazi ya wilaya.
5
Bi Eunice Mayongela akisisitiza jambo kuhusu Mkutao wa siku moja ulifanyika katika wilaya ya sengerema  kwa lengo la kuzungumzia maendeleo ya mradi  na changamoto zinaojitokeza.
6
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI akisisitiza Katika kipindi hiki Kivulini iliweza kutengeneza vitabu kwa ajili ya kuandikishia shauri, kutolea rufaa ,na kupata mrejesho wa rufaa kutoka kwa watoa huduma wengine na kugawanywa kwa wasidizi wa kisheria, Pia Kivulini iliweza kuwatengenezea vitambulisho wasidizi wa kisheria ili waweze kutambulikana kwa urahisi Zaidi katika jamii zao.
7
Baadhi ya Wasaidizi wa Kisheria toka wilaya ya Sengerema wakisikiliza kwa makini ripoti ya kiutendaji katika wilaya ya Sengerema, Mwanza.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa