Tone

Tone
Home » » MWANZA WAWASUBIRI MROPE,MUHANDO

MWANZA WAWASUBIRI MROPE,MUHANDO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Mwanza wameonyesha kumkubali mwimbaji wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Rebecca Malope, katika Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Mei 4 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Kwa mujibu wa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamash la Pasaka, Daniel Waziri, amefanya uchunguzi katika maeneo mbalimbali jijini humo na kugundua kwamba mbali ya Malope mwimbaji mwingine anayetakiwa kwa udi na uvumba na wakazi wa jiji hilo ni Rose Muhando.
Waziri alisema maeneo hasa yanayowataka waimbaji hao kwa udi na uvumba ni pamoja na vituo mbalimbali vya redio na televisheni jijini humo, ambao kwa tamko lao la pamoja wanawahitaji waimbaji hao na kutoa wito kwa kamati ya maandalizi kuwaleta waimbaji hao.
Aidha, Waziri alitoa wito kwa wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kujiandaa na tamasha hilo ambalo kwa jijini Mwanza litafanyika Mei 4 katika Uwanja wa CCM Kirumba, ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa