Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula amekemea vikali tabia
ya baadhi ya mameneja na wateja wa hoteli kuomba rushwa ya ngono kwa
wahudumu.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Umoja wa
Wafanyakazi wa Hoteli Kanda ya Ziwa (LHA) juzi, Mabula alisema suala la
rushwa ya ngono ni kikwazo cha maendeleo kwa sekta ya utalii.
“Lengo la LHA ni kuliangalia tabaka la chini
kwanza, halafu ndiyo mjiangalie mameneja, kwani mkiheshimu sekta hii
muhimu kwa pato la nchi, nasi tutafuata,” alisema na kuongeza kuwa
mameneja ni vijana wenye nguvu, wenye malengo na waliodhamiria kukomboa
sekta hii kwa kuwathamini watu ambao ni tabaka la chini, kwa kukomesha
rushwa ya ngono.
“Yapo masuala yanayowahusu wanataaluma, sisi
tunapaswa kuheshimu na kuthamini taaluma zao kama wanataaluma wenyewe
watajithamini na kujitambua. Tunafahamu changamoto zinazowakabili ila
naahidi Serikali inawaunga mkono kwa yale mazuri mnayoyafanya,” alisema.
Mabula alisema sekta ya hoteli ina changamoto
nyingi, ikiwamo uchache wa watumishi wenye maadili, hoteli zenye hadhi
ya nyota tano kwa kuwa wakipata wageni 1,000 hatuwezi kuwamudu kwa ubora
wa viwango..
Naye Katibu wa umoja huo, Shijani Mtunga alisema
lengo lao ni kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao za msingi kama
kutambulika kisheria.
“Kongamano la utalii la Februari liligusa suala la
kuongeza hoteli, kudumisha ufanisi na kuongeza ushindani, lakini haya
yote yanawezekana kama mameneja na wamiliki wataacha kuwanyanyasa
wafanyakazi ‘‘alisema Mtunga.
Mwenyekiti wa LHA, Dharmesh Talsania alisema lengo
lao lilikuwa kupata washiriki kutoka hoteli 30 kati ya 180 zilizopo
mkoani hapa, hata hivyo waliofanikiwa kusimamisha umoja huo wakiwa na
hoteli 17.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment