MBUNGE wa Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor (CCM),
amewahakikishia wananchi wa Ngudu na Mhalo kwamba ifikapo Machi
wataanza kupata majisafi kutoka Ziwa Victoria.
Alisema kuanzia Juni hadi Oktoba, wakazi wa kata mbalimbali ikiwemo
Hungumalwa, wataanza kupata umeme kupitia Mpango wa Umeme Vijijini
(REA).
Mansoor alisema hayo juzi alipofanya ziara ya ukaguzi miradi ya
maendeleo ikiwemo kuzungumza na waganga wa jadi ambapo aliweka wazi
kwamba tayari miradi hiyo ipo kwenye utekelezaji.
Mradi wa maji ni ahadi iliyotolewa hivi karibuni mjini Ngudu na
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Alitaja maeneo yatakayopatiwa umeme kuwa ni Mwang’halanga, Mhalo, Igogwa, Hundi, Lwande, Kikubiji na Mwamhala.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia
wakazi wake kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuwa sasa
maeneo mengi hayana umeme wala maji.
Aliahidi pia kuendelea kuchimba na kukarabati visima vya maji na
mabwawa kwa fedha zake ili kupunguza adha ya maji inayowakabili huku
akibainisha kwamba amechimba na kukarabati visima 30.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment