Home »
» CRDB YATUMIA MILIONI 50 KUKARABATI WARD YA WAJAWAZITO HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA
CRDB YATUMIA MILIONI 50 KUKARABATI WARD YA WAJAWAZITO HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA
 |
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akikata utepe kuashiria
ufunguzi ward ya wajawazito katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini
Mwanza ambapo CRDB iliifunga kwa muda ward hiyo ilikuifanyia ukarabati
madhubuti na kuwa ya kisasa zaidi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Ilemela Bi. Amina Masenza, Mkurugenzi wa BMC Prof. Charles Majinge,
Mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dr. Charles Kimei (aliyenyanyua mkono), Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na mmoja kati ya maafisa wa
CRDB. |
 |
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akifungua pazia la bango la
wadhamini katika hafla ya kukabidhi ward ya wajawazito Hospitali ya
Rufaa Bugando Mwanza iliyokarabatiwa na CRDB Benki. |
 |
Pia
CRDB imekabidhi mablanketi, vyandarua, vitanda na mashuka pamoja na
mapazia ya kusitiri huduma maalum kwa ward ya wajawazito Bugando. |
 |
Huduma
ya Afya ya mama na mtoto inakabiliwa na changamoto nyingi sana moja
wapo ni ugonjwa wa malaria ambao umekuwa moja ya vyanzo vikuu vya vifo
vya watoto nchini, kwa kuliona hilo CRDB wamehakikisha kila kitanda kina
neti yenye ukubwa wa kutosha. |
 |
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu akishiriki utandikaji mashuka na
blanketi katika ward ya wajawazito Hospitali ya Rufaa Bugando
iliyokarabatiwa na CRDB Bank.
|
 |
Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Bugando wakitandika 'kiprofesheno' zaidi... |
 |
Idadi
ya wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya na kuhudumiwa na
wataalamu wenye ujuzi imeongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2011 na
kufikia asilimia 65 mwaka 2013, hivyo mchango huu wa CRDB Bank
unaihamasisha jamii kukimbilia kwenye vituo vya afya kwani kuna uhakika
wa kupata huduma bora zaidi. |
 |
'Kiprofesheno' zaidi..!! |
 |
Ukarabati huu umegusa kila engo hadi hapa (sekta nyeti) |
 |
Mchango
wa magodoro, vitanda, matandiko, neti pamoja na mapazia ya kusitiri kwa
huduma za dharura ni kazi nzuri iliyofanywa na CRDB kwa vyumba vyote
vya ward ya wajawazito Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza. |
 |
Chumba kingine katika ward hiyo ya wajawazito BMC. |
 |
Furaha. |
 |
Blogger
G. Sengo akisaidizana na muuguzi wa ward ya Wajawazito Dr. Asha Juma
kutandika mashuka vitanda vya ward hiyo ya Hospitali ya Rufaa Bugando
jijini Mwanza iliyokarabatiwa na CRDB Bank. |
 |
"Asilimia
35 ya wakazi wa Mwanza huugua maralia kila mwaka, na malaria bado ni
ugunjwa tishio kwa mkoa wetu na nchi kwa ujumla, hivyo mchango wenu wa
ukarabati na vifaa vyake vikiwemo vyandarua ni kielelezo tosha cha benki
ya CRDB kuwakumbusha wananchi juuu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa
malaria" kauli ya mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo. |
 |
"Tukio
hili tunalifanya ikiwa ni hatua za kurejesha kiasi cha fungu la faida
kwa jamii, afya ya jamii inapoimarika ndipo watu wake wanapopata nafasi
ya kufanya kazi na kuwekeza kwenye mabenki yetu na hapo ndipo faida
inapopatikana"
"Jamii inapokuwa dhoofu kiafya basi kazi nazo
haziendi, uwekezaji wa tija unapungua na faida inakosekana, hivyo
tumeamua kuwekeza katika kuboresha afya ya jamii ili tuzidi kupata
faida" kauli ya Dr. Kimei. |
 |
"Mmekuwa
mfano, ninaamini sekta nyingine za fedha zitakuja kuwekeza hapa katika
hospitali hii ya pili kwa ukubwa nchini yenye kuhudumia watu takribani
milioni 18 ya wakazi wa kanda ya ziwa " kauli ya Prof. Majinge. |
 |
Mashuhuda na wafanyakazi wa CRDB walio hudhuria hafla hiyo. |
 |
Burudani toka Bujora Nyoka Dance. |
 |
Wadau haflani. |
 |
Kusanyiko haflani. |
 |
Shukurani za akina mama. |
0 comments:
Post a Comment