Home » » Bodi ya pamba yaweka mikakati kudhibiti ubora wa zao hilo

Bodi ya pamba yaweka mikakati kudhibiti ubora wa zao hilo

BODI ya Pamba  nchini imeweka mikakati mbalimbali ya kudhibiti viwango  vya ubora wa zao hilo ili kuhakikisha kuwa Pamba inayozalishwa na wakulima inapata bei nzuri na soko la  uhakika ndani na nje nchi.
Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ya kuelimisha wakulima  juu ya kilimo   bora  cha zao hilo,  pamoja na  Makampuni  yanayojihusisha na kilimo cha mkataba kutoa mbegu bora, pembejeo mbalimbali, ushauri wa kitaalamu pamoja na  vifungaishio
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa  zao  hilo mkoani Singida, mwakilishi wa Bodi ya Pamba bwana Epaphra Swai amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha zao hilo linamkoamboa mkulima.
Mgeni rasmi katika  ufunguzi wa mkutano huo mkuu wa mkoa wa Singida Dokta Parseko Kone amesema   ni vyema hatua hiyo iende pamoja na  kutafuta  wawekezaji katika sekta ya kuchambua pamba
Mbali na  changamoto ya  ubora, wastani wa uzalishaji wa  Pamba mkoani Singida ni Kg 350 kwa ekari, tofauti na kiwango cha  kitaifa  cha  Kg  1500.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa