Home » » UKEREWE YATANGAZA MKAKATI WA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MADAWATI

UKEREWE YATANGAZA MKAKATI WA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MADAWATI

WALIMU  wakuu wa  shule  za  msingi  katika wilaya  ya  Ukerewe, Mwanza  wameagizwa   kubuni  mbinu za  kuondoa   tatizo la madawati  katika shule zao  ikiwa ni pamoja na kutumia fedha  za ukarabati kutatua tatizo hilo.
Afisa  elimu   wa  elimu ya  msingi wa  wilaya  hiyo  Fidelis  Munyogwa  aliagiza hayo  jana katika shule ya msingi Ingongo  wakati  anapokea    madawati  62 mapya   yaliyotengenezwa  kwa fedha ya  ukarabati.
Alisema  wakati umefika sasa  wa kubuni  mbinu  mpya za  kukabili tatizo hilo  hasa kwa kutumia  miti  ya shule  pamoja na  fedha ya ukarabati  kutengeneza madawati  ya kutosha  ili kukidhi  maitaji makubwa yaliyopo.
Akifafanua  mbali ya  kupongea  uongozi wa shule hiyo ya Igongo pia aliutanganza utaratibu huo  kuwa  ndio mkakati na dira  ya   halmashauri  hiyo  ya kukaondoa kabisa  tatizo la muda mrefu  la upungufu wa madawati  shuleni.
Taarifa  zilizopo zinaonyesha  kuwa   shule za msingi  123 za wilaya hiyo zenye  wanafunzi  80,590  zinaitaji  madawati  37,404  lakini  yaliyopo   14,986.
Kufuatia  hali  hiyo  amesema  upo upungufu wa  madawati  22,058 hali ambayo  inathibisha kuwa   idadi kubwa ya  wanafunzi wanakaa chini na  pengine ndio sababu kubwa  ya  kushuka  kwa taalamu katika wilaya hiyo.
Kufuatia  hali  hiyo  Munyogwa  amesema   mwezi  uliopita halmashauri ya  wilaya hiyo  imepoke  sh. Mil. 11,363,636  za kutengeneza  madawati  ili kupunguza tatizo hilo  hata hivyo amesema  mbali ya  waisani, serikali  kuwajibika  katika hilo pia  chango wa jamii  unatakiwa  ili  kuwa  na nguvu ya pamoja  kutatua changamoto zilizopo katika sekta  ya elimu.
Naye  mwalimu  mkuu msaidi  wa shule ya  msingi  Igongo   Sedenslaus   Kalamagi  alisema   hiyo  yenye wanafunzi  805  inaitaji madawati  389 lakini yaliyopo  ni 176 baada ya  kutengeneza  madawati  hayo 62 mapya na sasa wanafunzi  130  wanakaa chini kwa kukosa madawati.
Alisema katika  kutekeleza mradi huo   wamevuna  miti 10 ya shule pamoja na  sh. 815,000   walizopokea  kwaajili ya ukarabati.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa